Monday, July 1, 2013

ROONEY: MTANITAMBUA OLD TRAFFORD!’


ROONEY_NA_FERGIE
                                                                                                                                                                                                                                                                                          WAYNE ROONEY ameamua kubaki na Mabingwa wa Manchester United kwa mujibu wa Magazeti kadhaa huko Uingereza hii leo.
Lakini, inadaiwa, atabaki kama ataongezewa Mkataba wake wa sasa kwa Maslahi anayoptata sasa.
Miaka mitatu iliyopita, mara baada ya kutangaza kutaka kuihama Man United, Klabu hiyo ilimpa Mkataba mpya uliokuwa ukimlipa Mshahara wa karibu Pauni 250,000 kwa Wiki na Mkataba huo umebakiza Miaka miwili sasa.
Pia, Rooney, Mwenye Miaka 27, ambae amevumishwa kutakiwa na Klabu kubwa England pamoja na Ulaya na ili kujiosha, ataitaka Klabu hiyo ithibitishe kuwa yeye hakuomba kuhama kama Meneja aliestaafu Sir Alex Ferguson alivyodai Mwezi Mei mara baada ya Ligi kumalizika.
Pia ripoti za Magazeti hayo ya Uingereza zimedai Rooney na Meneja mpya wa Man United, David Moyes, wameshakutana kwa siri ili kumaliza tofauti zilizokuwepo.
Licha ya kuvumishwa kuhama, ukweli ni kuwa Klabu nyingi za England, kama vile Arsenal na Chelsea, ambazo zilihusishwa na kumtaka endapo Man united ingekubali kumuachia, ingekuwa ngumu kumlipa Mshahara wake huo wa Pauni 250,000 kwa Wiki pamoja na Maslahi yake mengine.
Lakini, Klabu Tajiri zinazotamba kwa sasa Barani Ulaya, Monaco na PSG, uwezo huo wanao bila matatizo.
Wakati huo huo, Gwiji wa zamani wa Tottenham, Darren Anderton, amemtaka Wayne Rooney kubakia na Man United kwani hilo ni bora kwake.

0 comments:

Post a Comment