Saturday, June 8, 2013

TAIFA STARS LAZIMA KINUUKE LEO NCHINI MOROKO


Ni nafasi nyingine kwa timu ya Taifa ya Tanzaina kwampira wa miguu "Taifa Stars" kusaka ushindi wao wa kwanza nnje ya ardhi ya Tanzaia ikiwa chini ya Poulsein, pale watakapo kuwa wanasaka maboresho ya matumaini ya kushiriki kombe la dunia nhini Brazili mwakani.

Leo usiku saa 5 kwa saaa za Africa nashariki Taifa stars wana kibarua katika mji wa Marakesh pale watakapo karibishwa na wenyeji wa mji huo timu ya Taifa ya Morocco.

Taifa stars wakiwa wanapoint 6 nyuma ya vinara Ivory coast wenye point 7 wanahitaji ushindi wa aina yoyote kuendelea kukalia matumaini ya kufuzu kwa hatua ya mwisho ya kutafuta tiketi ya kucheza kombe la Dunia nnchini Brazili.

Taifa stars chini ya Jon Poulsein na Kim Poulsein hwajashinda mchezo wowote ule wa ugenini ukiondo michezo ya michuano ya CECAFA Chalenge Cup.

Chini ya kocha wa sasa Kim Poulsein, Taifa stars wamecheza michezo minne nnje ya ardhi ya Tanzania, miwili ikiwa ni ya mashindano dhidi ya Ivory coast na Msumbiji wakati mingine miwili ikiwa ni ya kirafiki dhidi ya Ethiopia na Sudan, ambapo wamepoteza miwili dhidi ya Ivory coast na Ethiopia wakati wakitoa sare dhidi ya Msumbiji na Sudani.

Taifa stars huenda leo wakaosa huduma ya beki Erasto Nyoni aliyepata jeraha katika mazoezi wakati timu ikiwa Ethiopia, huku wachezaji wengine wakiwa fiti kuelekea mchezo huo wa leo.

0 comments:

Post a Comment