Monday, June 10, 2013

MANCHESTER UNITED YA - YASAINI MKATABA WA NA MDHAMINI MPYA WA MIAKA MINNE NA BENKI YA INVEX YA MEXICO


Chicharito amechangia sana kuongezeka kwa umaarufu wa United nchini Mexico
• Patna wa kwanza wa huduma za kifedha America ya Kaskazini

INVEX wamepewa haki ya kipekee kutengeneza na kuuza credit cards zenye zilizotengenezwa kwa ajili ya washabiki millioni 24 wa United.


 Manchester United imesaini mkataba wa udhamini wa miaka minne na benki ya Mexico iitwayo INVEX.
Mkataba huu mpya utawapa INVEX haki za kuipekee kutengeneza na kuuza credit cards zenye zilizotengenezwa kwa ajili ya washabiki millioni 24 wa United.

Founded in 1991, INVEX ambayo ilianza kufanya kazi mwaka 1991 inatoa huduma nzuri na kuendelea kuwa bank inayoongoza huko Mexico - benki hiyo hutengeneza faida ya zaidi ya $252 million kwa mwaka na ina wateja zaidi ya 100,000 wanaotumia credit cards.
INVEX Manchester United Credit Card itatoa ofa kwa mashabiki wa United Mexico kwa faida na ofa za kipekee, zikiwemo punguzo la bei za bidhaa za United zinazouzwa online. Pia watakaokuwa na kadi hizo watakuwa wanapewa ofa ya jezi zilizosainiwa na wachezaji pamoja na tiketi za mechi. 

Mkurugenzi wa biashara wa United Richard Arnold alisema:
"Mexico inajulikana kwa mapenzi ya soka na Manchester United ina bahati ya kuwa na wapenzi wanaofikia millioni 24 ndani ya nchi hiyo. Hakuna anayeweza kusahau mapokezi makubwa tuliyoyapata wakati tulipokwenda Mexico mwaka 2010 wakati wa ufunguzi wa uwanja wa Chivas Stadium huko Guadalajara. Ushirikiano wetu na INVEX unaonyesha namna tulivyojikita katika kuwapa washabiki wetu hali ya kuwa na ukaribu nao popote pale walipo ndani ya Mexico. INVEX imetambua umashuhuri wa Manchester United ndani ya Mexico na kwa pamoja tutafanya kazi katika kuwaletea mashabiki wetu nafasi ya kuwa karibu klabu yao waipendayo pia na kuwapa faida za kifedha."

0 comments:

Post a Comment