KUNDI F ATAKAESONGA NI NIGERIA AU MALAWI.
SEP 6 KUAMUA, NI MTANANGE NIGERIA V MALAWI
JANA huko Windhoek, Nigeria walinusurika
kichapo toka kwa Namibia katika Mechi ya KUNDI F la Kombe la Dunia 2014
Kanda ya Afrika walipotoka Sare ya 1-1 lakini bado wako kileleni Pointi
2 mbele ya Malawi ambao mapema jana walitoka 2-2 na Kenya huko
Lilongwe.
ambayo itatoa Washindi watano
watakaoenda Brazil Mwaka 2014 kuamuliwa hapo Septemba 6 zitakapochezwa
Mechi za mwisho za Kundi kwa Nigeria kucheza na Malawi na Kenya kucheza
na Namibia.
KUNDI F
Nigeria –Pointi 9
Malawi - Pointi 7
Namibia -Pointi 5
Kenya - Pointi 3
MECHI ZA MWISHO:
Septemba 6
Nigeria v Malawi
Kenya v Namibia
Super Eagles walinusurika kipigo baada
ya Godfrey Oboabona kusawazisha Bao zikiwa zimebaki Dakika 7 baada ya
Deon Hotto Kavendji kuifungia Namibia Bao katika Dakika ya 77 kwenye
Mechi kali iliyochezwa Sam Nujoma Stadium huko Mjini Windhoek.
Nigeria sasa wanasafiri kwenda huko
Brazil kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayoanza Juni 15
na wao kufungua dimba na Tahiti hapo Juni 17 kwenye Mechi ya KUNDI B.
MAGOLI:
Malawi 2
-46' Ngalande
81' Ng’ambi
Kenya 2
52' Mohammed
89' Kayira [Kajifunga mwenyewe]
Namibia 1
77' Hotto
Nigeria 1
83' Godfrey Oboabona
Mapema huko Lilongwe, Malawi waliikosa Kenya baada ya Mchezaji wao Kayira kujifunga mwenyewe na kuipa Kenya Sare ya Bao 2-2.
Kenya na Namibia hazina nafasi tena ya kufuzu kutoka KUNDI F.
0 comments:
Post a Comment