Kuondoka
kwa wachezaji wengi kwenye ligi kuu ya Spain ni kitu kizuri kwa timu
yao ya taifa lakini sio jambo jema kwa ligi yao ya nyumbani, kwa mujibu
wa beki wa kimataifa wa Barcelona na Spain Gerard Pique.
Jesus Navas amekuwa
mchezaji mwingine wa timu ya taifa ya Spain kuhamia nje ya nchi hiyo
alipoondoka Sevilla na kuungana na mwenzie David Silva ndani
ya Manchester City.
Wachezaji tisa
wa kikosi cha sasa cha Spain kilichopo kwenye michuano ya Mabara huko
Brazil sasa wanacheza nje ya Spain - Laliga.
Vigogo Real
Madrid na Barcelona, klabu zinazoingiza mapato makubwa kabisa duniani
wana uwezo kuwa na wachezaji wazuri wawatakao na matokeo yake ndio
wanaotawala La Liga. Wana wachezaji 13 kwenye kikosi cha timu ya taifa.
Ingawa, vilabu
ambavyo vina matatizo ya kifedha kama Atletico Madrid, Valencia na
Sevilla vimekuwa vikilazimika kuuza wachezaji wao muhimu kutokana na
matatizo ya kifedha. www.Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment