Hii leo Kenya inajiandaa
kushuhudia mchuano wa kufa kupona kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles
wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi
Kasarani mjini Nairobi kuanzia saa kumi jioni saa za Afrika Mashariki.
Hii ni mechi ya mkondo wa pili kwa timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja walipocheza kwa mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana.
Mechi hii ni ya kundi la F ya kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Vijana wa kocha Stephen Keshi, wanatarajiwa kuendeleza ushindi wao hii leo wakijitafutia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michauno ya kombe la dunia nchini Brazil
Kwa vijana wa Eagles wanaosemekana kujiandaa vyema, wanafahamu kuwa ikiwa watashindwa basi itakuwa hasara kwao kwani hawataweza kwenda Brazil.
Licha ya kwenda sare mwezi jana, Nigeria inaingia kwenye mkondo huu bila ya kushindwa mechi yoyote ya makundi kati ya kumi na sita zilizocheza hadi kufikia sasa.
Wadadisi wanasema Eagles wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.
Nao upande wa Kenya chini ya ukufunzi wa Adel Amrouche, wako taabani kuboresha matokeo yao duni yanayowaweka katika nafasi ya tatu ili kwenda Brazil.
Wanaingia kwenye mechi hii wakiwa hawaonekani kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.
Kenya ingali kushinda mechi yoyote ya kufuzu baada ya kwenda sare tasa dhidi ya Malawi pamoja na kwenda sare ya bao moja dhidi ya Nigeria.
Kwa matokeo, Nigeria wako mbele kwenye F wakiwa na pointi 5 wakifuatwa na Mawi wenye pointi tano pia. Namibia wana pointi tatu huku Kenya ikiwa na pointi mbili.
14:50 PM :Shamra shamra zimeanza kupamba moto katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani. Mwandishi wa BBC ambaye yuko katika uwanja huo Odeo Sirari, anasema kuw mashabiki wanzidi kumiminika uwanjani. Milango ya uwanja ilifunguliwa rasmi majira ya saa tano asubuhi
14:58 PM: Mojawapo ya mabango ya mashabiki uwanjani yana bendera ya Kenya na maandishi ''Oga you are finished'' kwa maana kuwa Nigeria itashindwa . Odeo anasema hayo ni maoni ya mashabiki wa Nigeria uwanjani
Mechi inatarajiwa kuanza saa kumi kamili. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria
0 comments:
Post a Comment