BREAKING NEWS: AMRI KIEMBA ASAINI SIMBA KWA MILLIONI 35
Hatimaye mazungumzo baina ya Klabu ya Simba na mchezaji Amri Kiemba yamemalizika kwa pande hizo mbili kukubaliana kuongeza mkataba mpya.
Mchana
wa leo Simba ilikuwa kwenye jitihada nzito kuhakikisha inamzuia Kiemba
kusaini Yanga kwa kumpa ofa nono ya mkataba mpya, Kiemba alikuwa
akihitaji kiasi cha millioni 38 ili asaini msimbazi lakini baada ya
mazungumzo marefu Kiemba amekubali kusaini kwa kiasi cha millioni 35 kwa
miaka miwili.
Pia Kiemba atakuwa analipwa
mshahara wa millioni 2 kwa mwezi. Alisaini mkataba huo mbele ya kaimu
makamu mwenyekiti Mzee Kinesi.
0 comments:
Post a Comment