Friday, February 14, 2014

AJALI YA PIKIPIKI, ILIYOMPATA MSANII WA FLAMU KUELEKEA SIKUKUU YA WAPENDANAO ALIMANUSULA!!!



AJALI mbaya aliyoipata msanii wa filamu, Tito Zimbwe hivi karibuni ilikuwa imfanye apoteze maisha yake kutokana na namna ilivyotokea.

Rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, ajali aliyoipita Tito kupona kwake ilikuwa ni Mungu tu kwani waliomuokoa walisema ameponea kwenye tundu la sindano.
“Aisee ilikuwa ni ajali mbaya sana, ilikuwa mida ya saa tano usiku, alikuwa akitokea Kigogo kwenda Kinondoni akiendesha pikipiki, alipofika maeneo ya Shule ya Msingi Lutihinda akakutana na tuta ambalo lilimfanya apate ajali, ni Mungu tu kwa kweli.”
Baada ya ajali hiyo Tito alipata majeraja sehemu mbalimbali za mwili na alipelekwa kwenye Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni ambapo inaelezwa anaendelea vizuri.

0 comments:

Post a Comment