Monday, January 20, 2014

Fahamu kwa nn Ronaldo Alitoa chozi!!!!!!


KWA wanaomtambua tangu utoto wake, alichokifanya Jumatatu iliyopita kitendo cha Cristiano Ronaldo alidondosha chozi............
aliponyakua tuzo yake ya pili ya Mwanasoka Bora wa Dunia, lakini kitendo cha kulia na kutokwa machozi ni kitu alichokifanya sana utotoni kutokana na kukabiliwa na ugumu wa maisha.
Akiwa amezaliwa katika mji wa kimasikini sana, Madeira huko Funchal, Ureno alikuwa na sifa moja ya kulia kila mambo yake yalipokwama, lakini kwenye tukio lile la wiki iliyopita, Ronaldo alidondosha chozi la furaha baada ya kutajwa mshindi wa Ballon d’Or tuzo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa mbele ya Lionel Messi na Franck Ribery.
Ronaldo utotoni
Alikulia katika mji wa milima mingi kisiwani kwenye eneo lililoitwa Santo Antonio, utotoni Ronaldo alikuwa mtoto wa mama (legelege). Akiwa wa nne kwenye familia ya Dolores na Dinis, mimba ya Ronaldo ilikuwa ya bahati mbaya.
Mama yake alikuwa mpishi na baba yake alikuwa mtunza bustani wa manispaa, ambaye alikuwa ameathirika sana kwa ulevi kabla ya kufariki 2005.
Misosi ilikuwa adimu sana nyumbani kwa kina Ronaldo.
Alipozaliwa mama yake alimpa jina la Cristiano, baba yake akampa Ronaldo ikiwa ni jina la Ronald Reagan (Mwigizaji filamu na rais wa zamani wa Marekani, ambaye Dinis alikuwa kipenzi chake).
Baada ya kuandamana na baba yake kwenda kwenye klabu ya kijijini kwao, Andorinha, Ronaldo akaanza kuwa na mapenzi ya soka na kipindi hicho alikuwa akicheza na binamu yake, Nuno. Alipoanza soka, Ronaldo hakurudi tena nyuma.
Aanza kucheza beki
Francisco Afonso, mwalimu wa shula ya msingi, ambaye alikuwa kocha wa kwanza kumnoa Ronaldo, alifichua ukweli kuhusu staa huyo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno baada ya kudai mwanzoni fowadi huyo alianzia kucheza beki. “Alionekana kuwa na kitu tangu utoto wake, alikuwa na mwili mdogo sana, lakini alihitaji kufanya kitu,” anasema.
“Alianza kucheza beki kabla ya kuamua kupanda mbele kwa sababu alitaka kushiriki kila kitu. Alikuwa mahiri kwenye miguu yote na alikuwa na kasi sana kitu ambacho aliendelea kukifanyia mazoezi muda wote na kuwa bora zaidi. Soka ikawa ndiyo kila kitu kwake, asipocheza alikuwa kama mgonjwa.” posted by http://thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment