Monday, October 21, 2013

ZA HIVI PUNDE: Marehemu Julius Nyaisanga kuagwa Moro Leo na Dar es salaam kesho



Aliyekuwa mtangazaji maarufu wa redio nchini Tanzania, Julius Nyaisanga (pichani katikati), ambaye alifariki jana mjini Moro, anatarajiwa kuagwa leo mjini humo na maiti yake kusafirishwa kwenda Dar kwa ajili ya kuagwa kesho na wakazi wa jiji la Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mchana huu, uamuzi huo umefikia kati ya Kamati ya Mazishi ya Morogoro na uongozi kutoka Serikalini ambao waliomba ufanyike utaratibu huo ili kuwawezesha watu wengi kutoa heshima zao za mwisho kwa mtangazaji huyo aliyeishi kwa miaka mingi jijini.
Posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment