Monday, September 30, 2013

WENGER PRESHA BADO NINAYO: ASISITIZA KUZUNGUMZIA UBINGWA SASA NI UPUUZI!!!!

WENGER-PROFESA

Arsene Wenger amesisitiza kuwa ni upuuzi kuzungumzia hivi sasa kuhusu Arsenal kutwaa Ubingwa licha ya kuwa wao ndio wanaongoza baada ya kushinda Mechi 5 kati ya 6 za Ligi Kuu England walizocheza.

Arsenal wako kileleni Pointi 2 mbele baada ya Jumamosi kushinda 2-1 Ugenini walipoichapa Swansea City na huo ni ushindi wao wa tano mfululizo toka kichapo cha Mechi ya kwanza kabisa walipofungwa 3-1 na Aston Villa.

Akiongea kabla Mechi yao ya Jumanne ya KUNDI F la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, watakayochezea kwao Emirates na Napoli, Wenger alisema: “Tunataka uwiano mzuri kuhusu nia na unyenyekevu. Kuzungumzia Ubingwa leo hii ni upuuzi! ”
Wenger alisema walipofungwa na Villa kwenye Mechi ya kwanza yeye hakuwa na wasiwasi na kufafanua: “Watu wanasahau tulikuwa kwenye mbio ndefu za kutofungwa tangu Machi na ukichukulia hiyo kufungwa na Villa ni Mechi moja tu kati ya 21. Na Watu kuanza kupiga kelele wakati huo ni mchanganyiko wa vitu vingi, hatukununua Mchezaji, hatujachukua Ubingwa muda mrefu na ukweli kuwa tumefungwa Mechi. Vitu vyote hivyo vilileta mlipuko wa hasira lakini kufungwa ni bahati mbaya na tumejirekebisha!”
Moja ya sababu ya Arsenal kufanya vizuri ni fomu nzuri ya Kiungo wao Aaron Ramsey ambae ameshafunga jumla ya Bao 9 na 5 ni katika Gemu 4 za mwisho na pia Straika Olivier Giroud ambae mpaka sasa ameshafunga Bao 5.
LEO GOODISON PARK: NI EVERTON v NEWCASTLE!!
Leo Saa 4 Usiku kwenye Uwanja wa Goodison Park ipo Mechi moja ya Ligi Kuu England kati yaBPL2013LOGOWenyeji Everton na Newcastle.
Everton ndio Timu pekee kwenye Ligi ambayo haijafungwa na pia tangu Mwezi Machi hawajafungwa Bao lolote kwenye Ligi Uwanjani kwao Goodison Park.
Mara ya mwisho Everton kufungwa Bao Uwanjani hapo ni pale Robson Kanu alipoifungia Reading na tangu wakati huo Saa 7 na Dakika 6 za Mechi zimeshapita bila kufungwa Bao hata moja huku West Ham, Fulham, QPR, Manchester City, Stoke City, West Brom na Chelsea zikishindwa kupata Bao lolote.
Mwaka huu wote wa 2013, ni Wigan pekee, ilipokuwa chini ya Meneja wa sasa wa Everton, Roberto Martinez, ndio iliyoifunga Everton Uwanjani hapo.
Lakini Rekodi ya Newcastle Uwanjani Goodison Park sio nzuri kwani wameshinda Mechi moja tu kati ya 10 walizocheza mwisho na katika Mechi ya mwisho Msimu uliopita walitoka Sare 2-2.
Uso kwa Uso
-Newcastle wameshinda  Mechi moja tu kati ya 10 walizocheza mwisho na hiyo ilikuwa Miaka mitatu iliyopita pale Hatem Ben Arfa, ikiwa ni Mechi yake ya kwanza tu tangu ajiunge na Newcastle, alipopiga mkwaju wa Mita 25 na kufunga.
-Klabu hizi zimeshakutana mara 164 na Everton kushinda mara 65 na Newcastle mara 64.
LEO GOODISON PARK: NI EVERTON v NEWCASTLE!!
RATIBA: YA LEO
BPL: LIGI KUU ENGLAND
Jumatatu 30 Septemba
22:00 Everton v Newcastle United

RATIBA:
BPL: LIGI KUU ENGLAND
Jumatatu 30 Septemba
22:00 Everton v Newcastle United
Jumamosi 5 Oktoba
14:45 Manchester City v Everton
17:00 Cardiff City v Newcastle United
17:00 Fulham v Stoke City
17:00 Hull City v Aston Villa
17:00 Liverpool v Crystal Palace
19:30 Sunderland v Manchester United
Jumapili 6 Oktoba
15:30 Norwich City v Chelsea
15:30 Southampton v Swansea City
18:00 West Bromwich Albion v Arsenal
18:00 Tottenham Hotspur v West Ham United
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
6
6
15
2
Liverpool
6
4
13
3
Tottenham
6
4
13
4
Chelsea
6
4
11
5
Southampton
6
3
11
6
Man City
6
7
10
7
Hull
6
-1
10
8
Everton
5
2
9
9
Aston Villa
6
1
9
10
West Brom
6
1
8
11
Cardiff
6
-1
8
12
Man Utd
6
0
7
13
Swansea
6
-1
7
14
Norwich
6
-2
7
15
Stoke
6
-2
7
16
Newcastle
5
-3
7
17
West Ham
6
-1
5
18
Fulham
6
-5
4
19
Crystal Palace
6
-6
3
20
Sunderland
6
-10
1
Posted by Thesuperonenews.blogspot .com

0 comments:

Post a Comment