MASKINI Daz Baba! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari ya
kusikitisha ya msanii huyo ambaye jina lake kamili ni David Jacob
kunaswa akiwa amezima mjini hapa huku ulevi wa kupindukia ukidaiwa kuwa
chanzo.
|
hii ni moja ya picha inavyomuonesha kipindi cha nyuma alivyokuwa akionekana tofauti na sasa |
Daz Baba au Daz Mwalimu asubuhi ya Agosti 5, mwaka huu alinaswa na
kamera za gazeti hili akiwa hajitambui kwenye eneo maarufu kwa jina la
Itigi lililopo nje ya Stendi ya Mabasi ya Msamvu ikidaiwa kuwa alifika
mitaa hiyo tangu usiku wa jana yake.
Awali chanzo chetu cha habari kilitupigia simu na kutueleza juu ya
kuzimika kwa msanii huyo aliyekuwa akiunda Kundi la Daz Nundaz Family na
baada ya paparazi wetu kufika eneo la tukio ambalo ni maarufu kwa
biashara haramu ya ukahaba, lilibaini kuwa ni yeye na wasamaria wema
walikuwa wakijaribu kumuamsha
“Huyu atakuwa amelewa sana na inawezekana katumia madawa ya kulevya
au kawekewa madawa kwenye bia. Dah! Inasikitisha sana kwa msanii kama
huyu ambaye huko nyuma alikuwa aking’ara kwenye anga la muziki,”
alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa eneo hilo.
|
kwa muda uliopita nunda ailikuwa akionekana hivi |
Hata hivyo, jitihada za kumuamsha ziligonga ukuta na mpaka pandaparazi
wetu anaondoka eneo la tukio bado msanii huyo alikuwa hajitambui na
mfukoni hakuwa na kitu, ikiashiria kuwa wahuni walimkomba kila kitu.
posted by Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment