Saturday, August 3, 2013

WENGER PRESHA INAPANDA NA KUSHUKA!!


EMIRATES_CUP





    












 HUKU akikiri kuwa ipo presha kubwa ya kununua Wachezaji kwenye Kipindi hiki cha Uhamisho, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema watafanya ununuzi kwa Mchezaji anaestahili tu na si kuvamia Soko na kununua Mchezaji ili mradi wametoa Fedha nyingi.
Wakiwa Wikiendi hii wapo Nyumbani kwao Emirates wakicheza Mashindano ya Kombe lao Emirates Cup kwa kuanza kucheza na Napoli Jumamosi, Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, aliahidi mwishoni mwa Msimu uliopita kuwa Arsenal wataonyesha makucha yao kifedha kwa kununua Mchezaji wa Bei mbaya Msimu huu unaokuja lakini hadi sasa bado hilo halijatimia.
EMERATES CUP
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Agosti 3
15:00 Galatasaray Spor Kulübü – Turkey v FC Porto - Portugal
17:20 Arsenal FC – England v      Napoli - Italy
Jumapili Agosti 4
15:00 Napoli – Italy v FC Porto - Portugal
17:20 Arsenal FC – England v Galatasaray Spor Kulübü - Turkey
Arsenal walimuwania Straika wa Real Madrid, Gonzalo Higuain, lakini wakashindwa na Mchezaji huyo kwenda Napoli kwa Meneja Rafael Benitez.
Pia, walimtaka Luis Suarez wa Liverpool na kutoa Ofa ya Pauni 40,000,001 lakini hii nayo imekataliwa.
Hata hivyo, Jana Wenger alisema: “Tunafanya kazi kwa bidii kuimarisha Kikosi na si kwa Suarez tu bali wengine! Siku zote tunataka kufanya uamuzi sahihi kwa Klabu!”
Kwa Kipindi hiki cha Uhamisho, Arsenal wamempata Mchezaji mmoja tu, tena kwa Uhamisho wa bure, Chipukizi wa Klabu ya France Auxerre, Yaya Sanogo

0 comments:

Post a Comment