WAKATI
Staa mpya wa Monaco, Radamel Falcao, akisakamwa na skandali la
kupunguza Miaka ya Umri wake, Winga wa Stoke City, Jermaine Pennant,
amegomewa kuingia USA kwa sababu ya kuwa na Rekodi ya Kihalifu.
Pennant azuiwa kuingia USA
Jermaine Pennant ameshindwa kuingia
Nchini USA ili kuwa pamoja na Timu yake Stoke City kwenye Ziara ya
matayarisho ya Msimu mpya na imebidi abaki England kuendelea na Mazoezi
binafsi.
Hii ni mara ya pili kwa Pennant
kukatiliwa kuingia USA na mara ya kwanza ilikuwa ni Mwaka Jana na sababu
inayotolewa ni kwamba Mchezaji huyo alihukumiwa na kupewa Adhabu ya
Uhalifu kwa Kosa la kuendesha Gari akiwa amelewa.
Kwa mujibu wa Marekani, Nchi hiyo
imetaka uhakika kuwa Mchezaji huyo sasa amesafishika ili kumruhusu
kuingia kitu ambacho hakikuthibitishwa kwa Mamlaka husika.
Umri wa Radamel Falcao
Straika mpya wa Monaco Radamel Falcao
amekanusha habari zilizozagaa kuwa Umri wake ni Miaka 29 na sio 27 kama
anavyojitangaza mwenyewe.
Hivi karibuni, Falcao alijiunga na Monaco kwa Dau la Pauni Milioni 53 huku Umri wake rasmi ukitajwa kuwa ni Miaka 27.
Lakini, Mchezaji huyo kutoka Uruguay,
amevumishwa huko kwao Marekani ya Kusini kuwa Umri wake halali ni Miaka
miwili zaidi kitu ambacho kingeathiri sana Dau lake la Uhamisho.
Mwenyewe Falcao amestushwa na habari
hizo na alilazimika kuandika kwenye Ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter:
“Nimeshangazwa na habari kwenye Vyombo vua Habari kuhusu Umri wangu. Ni
upuuzi mkubwa. Nataka kukanusha ishu hii kwa ujumla!
0 comments:
Post a Comment