USHIRIKI
wa Timu za Tanzania kwenye Mashindano ya CECAFA ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, KAGAME CUP yaliyokuwa yaanze Juni 18, umeingia kwenye
utata mkubwa kufuatia Klabu za Yanga na Simba kuvunja Kambi zao.
Akiongea huko Dodoma hiyo Jana, Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, alisema
Serikali imepata uthibitisho toka Serikali ya Sudan kwamba Timu za
Tanzania zitapewa ulinzi wa kutosha na kuhakikisha usalama wao.
Tanzania ilikuwa iwakilishwe na Timu 3,
Yanga, kama Mabingwa Watetezi wa Kagame Cup, Simba kama Mabingwa
Tanzania Bara Msimu wa 2011/12 na Falcon FC ya Zanzibar kama Mabingwa wa
Zanzibar Msimu uliopita.
Hata hivyo, hadi sasa haijulikani kama
Timu hizo zitashiriki, hasa Yanga na Simba, ambazo mara baada ya
kuambiwa na Serikali kwamba huko Darfur hamna uhakika wa usalama wao,
Timu hizo zilivunja Kambi za Mazoezi na kuwapa Likizo Wachezaji wao.
Mbali ya Timu za Tanzania kujitoa, Tusker FC ya Kenya pia ilijitoa ikihofia usalama wake.
Vile vile, hiyo Jana Katibu Mkuu wa
CECAFA, Nicholas Musonye, alishatangaza kubadilisha Ratiba na kuziingiza
Electric Sports ya Chad [Si Mwanachama wa CECAFA] na URA ya Uganda.
Timu ambazo zimebaki kushiriki
Mashindano hayo ni: Al Ahly Shandi (Sudan), Al Nasir (South Sudan),
Al-Hilal Kadugli (Sudan), Express FC (Uganda), URA FC (Uganda), Ports FC
(Djibouti), Vital’O (Burundi), Merriekh El Fasher (Sudan), APR
(Rwanda), Elman (Somalia), Rayon Sport (Rwanda) na Electric Sport
(Chad).
TUSKER YA KENYA ILISHAJITOA KUHOFIA USALAMAThesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment