Tuesday, June 11, 2013

CHUO CHA MAKOCHA NCHINI LEO CHA SEMA KITU.




Ujumbe kutoka Chuo cha Makocha nchini Ireland umewasili jana, katika klabu ya Kitayosce ya Mjini Moshi kwa ajili ya kushirikiana na kupeana uzoefu.

Ujumbe huo ni wa makocha  6 umewasili na kuanza kazi ya kuinoa timu ya Kitayosce katika uwanja wa King George Memorial, uliopo Soweto Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Uongozi wa Kitayosce FC umesema makocha hao watakaa na timu hiyo kwa muda wa siku 14 kwa ajili ya kuifundisha hasa ikizingatiwa inajianda na michuano mitatu.

Uongozi wa Kitayosce umeitaja michuano hiyo kuwa ni Mkombozi Cup, Marealle Cup na Ligi ya Mkoa.

Makocha waliowasili klabuni hapo Conall Walsh, Adam Crowther, Andrew Grehan, John Harrington, Darragh MacGill na Keith McNamara.

Kocha wa Klabu ya Kitayosce Hamad Haule amesema ujio wao utamsaidia kuongeza nguvu katika vikosi vyake katika michauano ijayo.

Hamad ameongeza kusema ujio huo ni wa mara ya pili, itakumbukwa kwamba walikuja mwaka jana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na Klabu yake ilifaidi ujio wao.

Leo ujumbe huo wa makocha umeingia siku ya pili ya mazoezi na Kitayosce FC kwa mazoezi ambapo wachezaji 30 wapo chini yao kwa kuwaongeza vitu adimu katika mchezo wa soka.

0 comments:

Post a Comment