Saturday, June 8, 2013

Sumaye aweka mgomo juu ya serikali tatu Tanzania

Tluway_Sumaye
Waziri mkuu wa zamani katika awamu ya tatu Fredick Sumaye ameipinga hoja ya serikali tatu katika rasimu ya katiba mpya ya Tanzania.

Akiongea katika kipindi cha mahojiano na BBC Sumaye anasema ‘Serikali tatu ni mzigo kwa Tanzania ambayo uchumi wake si mkubwa. Hata waasisi wa Muungano waliliona ilo suala’.
Hoja ya kuwa na serikali tatu ambayo ni Tanzania, Tanzania bara na Zanzibar imeongelewa sana toka rasimu ya katiba mpya ilipozinduliwa.

0 comments:

Post a Comment