Mwanzoni mwa wiki hii Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilizindua rasimu ya Katiba Mpya iliyopendekeza kuwapo kwa mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa utawala nchini, huku yakionekana kuwa machungu kwa chama tawala cha CCM.
Tayari CCM kimetangaza kufanya mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri
Kuu ya Taifa ya chama hicho ili kuichambua na kujadili kwa kina rasimu
hiyo ya Katiba Mpya.
Jana vyombo vya habari vilimnukuu Katibu Mkuu wa chama hicho
Abdulrahman Kinana katika mkutano wake na waandishi wa habari akisema
kuwa wataichambua na kuijadili rasimu hiyo.
Pamoja na mambo mengine, rasimu hiyo ya Katiba Mpya imependekeza
kuwapo kwa Serikali tatu; Shirikisho la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Zanzibar, kuruhusiwa kwa
mgombea binafsi na kufutwa kwa viti maalumu vya ubunge.
Mapendekeo hayo yametolewa ikiwa ni miezi sita tangu vyama mbalimbali
vya siasa kuwasilisha maoni yao kwa tume hiyo inayoongozwa na Jaji
Joseph Warioba na kupendekeza mambo mbalimbali ikiwamo muundo wa
Serikali, Uchaguzi Mkuu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mapendekezo ya CCM
Katika mapendekezo yake CCM walitaka ubaki mfumo wa Serikali mbili
kama ilivyo sasa, ikieleza kuwa hauna gharama, huku kikieleza kwamba
uzoefu katika nchi nyingi za Afrika unathibitisha kushindwa kwa mfumo wa
Serikali tatu na ule wa Serikali ya Shirikisho (Federation government).
Hata hivyo, mapendekezo ya rasimu hiyo yanaonyesha kuwa Jamhuri ya
Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye Serikali tatu na kwamba
shughuli zote za muungano zitasimamiwa na Serikali, Bunge na Mahakama ya
Jamhuri ya Muungano, hivyo kukifanya CCM kuanguka katika maoni kuhusu
suala hilo.
CCM ilipendekeza sera ya dola kutokuwa na dini rasmi, bali iruhusu
kila mtu kuwa na uhuru wa kufuata dini anayoitaka mwenyewe, jambo ambalo
limebaki kama lilivyo katika mapendekezo ya rasimu hiyo.
Chama hicho kimeonekana kukwama pia katika mapendekezo yake ya
kuupigia debe mfumo wa sasa wa rais kushinda kwa wingi wa kura (simple
majority) kwa maelezo kuwa hauna gharama pamoja na kutaka wananchi wawe
na haki ya kuhoji uchaguzi wa rais.
Lakini, mapendekezo katika rasimu hiyo yanaeleza kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano atatangazwa baada ya kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura
zote na endapo hakutakuwa na mshindi, walioshika nafasi ya kwanza na ya
pili watarudia uchaguzi ndani ya siku 60.
CCM kilipendekeza mawaziri wasitoke nje ya Bunge, huku kikitaka
kuongezwa kwa wigo wa viongozi wanaoteuliwa na rais na kupitishwa na
Bunge kama ilivyo kwa waziri mkuu.Mapendekezo mengine ya chama hicho ambayo hayakupitishwa ni kuanzishwa kwa utaratibu utakaoshirikisha Bunge katika uteuzi wa baadhi ya vyombo vya utendaji ikiwemo tume ya uchaguzi na kutokuwepo mgombea binafsi .
Mbali na hayo, chama hicho pia kilitaka uwepo ukomo wa idadi ya
wabunge ili kuzuia uwezekano wa kuongeza majimbo bila kuzingatia vigezo
mahsusi na uwezo wa taifa.
Kuhusu wabunge wa viti maalumu CCM ilitaka idadi ya wabunge hao
itokane na asilimia ya idadi ya viti iliyopata chama baada ya kushinda
uchaguzi.
Kuhusu kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa rais, CCM ilitaka
uwepo utaratibu maalumu wa kupinga matokeo hayo na siyo mahakamani.
Chadema
Kwa upande wa Chadema kilipendekeza kuanzishwa kwa utawala wa majimbo
yasiyozidi kumi ili kuleta uwiano katika matumizi ya rasilimali kwenye
maeneo yote ya nchi. Hata hivyo, rasimu hiyo ilipendekeza kutokuwepo kwa
Serikali za majimbo ikieleza kungechochea mgawanyiko ambao ungejengwa
kwa misingi ya udini, ukabila na ukanda.
Chadema pia kilipendekeza umri wa kugombea ubunge ushushwe hadi miaka
18 ili kutoa nafasi kwa mtu yoyote kuwa na haki ya kupiga au kupigiwa
kura, lakini rasimu hiyo imeeleza kuwa umri wa mtu kugombea ubunge ni
miaka 21 huku ikitaja umri wa kugombea urais kuwa ni kuanzia miaka 40.
Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chama hicho
kilipendekeza iwe na wajumbe 25 kati yao 15 watokane na vyama vyenye
uwakilishi bungeni na wateuliwa kwa uwiano wa wabunge walioko bungeni,
wengine watoke kwenye asasi za kiraia, vyama vya wakulima, jumuiya za
kidini na vyama vingine vya siasa visivyo na uwakilishi bungeni na
mwenyekiti na makamu wake wateuliwe na wajumbe wenyewe.
Katika hilo chama hicho kimekwama kwani rasimu imependekeza kuwa wajumbe wa tume hiyo watateuliwa na rais.
Mapendekezo ya chama hicho ambayo yamepitishwa na tume ni pamoja na
kuwepo kwa Serikali tatu, matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani.
CUF
Ilipendekeza kuwapo Katiba tatu zitakazoongoza Serikali za
Tanganyika, Zanzibar na Muungano jambo ambalo limependekezwa pia na
Rasimu ya Katiba Mpya.Mapendekezo mengine ya chama hicho ambayo hayakupitishwa ni kuanzishwa kwa utaratibu utakaoshirikisha Bunge katika uteuzi wa baadhi ya vyombo vya utendaji ikiwemo tume ya uchaguzi na kutokuwepo mgombea binafsi .
Mbali na hayo, chama hicho pia kilitaka uwepo ukomo wa idadi ya
wabunge ili kuzuia uwezekano wa kuongeza majimbo bila kuzingatia vigezo
mahsusi na uwezo wa taifa.
Kuhusu wabunge wa viti maalumu CCM ilitaka idadi ya wabunge hao
itokane na asilimia ya idadi ya viti iliyopata chama baada ya kushinda
uchaguzi.
Kuhusu kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa rais, CCM ilitaka
uwepo utaratibu maalumu wa kupinga matokeo hayo na siyo mahakamani.
Chadema
Kwa upande wa Chadema kilipendekeza kuanzishwa kwa utawala wa majimbo
yasiyozidi kumi ili kuleta uwiano katika matumizi ya rasilimali kwenye
maeneo yote ya nchi. Hata hivyo, rasimu hiyo ilipendekeza kutokuwepo kwa
Serikali za majimbo ikieleza kungechochea mgawanyiko ambao ungejengwa
kwa misingi ya udini, ukabila na ukanda.
Chadema pia kilipendekeza umri wa kugombea ubunge ushushwe hadi miaka
18 ili kutoa nafasi kwa mtu yoyote kuwa na haki ya kupiga au kupigiwa
kura, lakini rasimu hiyo imeeleza kuwa umri wa mtu kugombea ubunge ni
miaka 21 huku ikitaja umri wa kugombea urais kuwa ni kuanzia miaka 40.
Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chama hicho
kilipendekeza iwe na wajumbe 25 kati yao 15 watokane na vyama vyenye
uwakilishi bungeni na wateuliwa kwa uwiano wa wabunge walioko bungeni,
wengine watoke kwenye asasi za kiraia, vyama vya wakulima, jumuiya za
kidini na vyama vingine vya siasa visivyo na uwakilishi bungeni na
mwenyekiti na makamu wake wateuliwe na wajumbe wenyewe.
Katika hilo chama hicho kimekwama kwani rasimu imependekeza kuwa wajumbe wa tume hiyo watateuliwa na rais.
Mapendekezo ya chama hicho ambayo yamepitishwa na tume ni pamoja na
kuwepo kwa Serikali tatu, matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani.
CUF
Ilipendekeza kuwapo Katiba tatu zitakazoongoza Serikali za
Tanganyika, Zanzibar na Muungano jambo ambalo limependekezwa pia na
Rasimu ya Katiba Mpya.Chama hicho pia kilipendekeza mgombea binafsi katika nafasi ya urais, kupunguzwa kwa madaraka ya rais na rais apatikane kwa kupata zaidi ya asilimia 50.
0 comments:
Post a Comment