Wednesday, June 12, 2013

MONTOLIVO KUWA NAHODHA MPYA SAN SIRO AC MILAN WATHIBITISHA WAMEMUACHA AMBROSINI -

AC Milan CEO Adriano Galliani amethibitisha kwamba nahodha wa klabu hiyo  Massimo Ambrosini ataondoka San Siro pindi mkataba wake utakapoisha mwezi huu baadae.

Kiungo huyo mwenye miaka 36 alijiunga na Rossoneri akitokea Cesena mwaka 1995 na amekuwa na klabu hiyo tangu wakati huo, japokuwa aliondoka kwa mkopo kwenda Vicenza kuanzia 1997-98.
 

Alitajwa kuwa nahodha wa klabu hiyo mnamo mwaka 2009 kufuatia kuondoka kwa Paolo Maldini lakini sasa muda wake ndani ya Giuseppe Meazza umefikia mwisho.

"Milan itaachana na Ambrosini," Galliani aliiambia Sky Italia.

"Nahodha wetu ajaye atakuwa Riccardo Montolivo ikiwa Christian Abbiati atakubali."

0 comments:

Post a Comment