Tuesday, June 11, 2013

Ahmed Mido wa Misri astaafu Soka.


.

Zamalek's Ahmed Hossam "Mido" celebrates a goal during their friendly soccer match against Atletico Madrid at Cairo Stadium


Mido anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wa Kiafrika waliowahi kucheza soka kwenye vilabu vingi barani ulaya akiwa amecheza kwenye ligi za Uholanzi, Ubelgiji , Hispania,Ufaransa,England ,Italia na nchini kao Misri ambapo amecheza kwenye klabu za Zamalek alikoanzia maisha yake ya soka wakati akiwa na miaka 16, Gent ya Ubelgiji, Ajax Amsterdam ya Uholanzi,Celta Vigo ya Hispania , Olympique Marseile ya Ufaransa,As Roma ya Italia ,Tottenham Hotspurs , Middlesborough,Wigan Athletic,West Ham United na  Barnsley zote za Engand .
Mido amewahi kuichezea timu yake ya taifa ya Misri kwenye mechi 51 ambapo alifunga mabao 20 huku akiwa sehemu muhimu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2006 . Hata hivyo Mido atakumbukwa kwa sababu mbaya kwenye timu ya taifa yakiwemo matukio kadhaa ya utovu wa nidhamu kama kukataa kutolewa uwanjani na kumtolea kocha wake Hassan Shehata maneno machafu baada ya kutolewa uwanjani wakati wa mchezo wa fainali ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2006 .
Mido amewahi kutwaa mataji manne kwenye klabu za Ajax Amsterdam na Zamalek pamoja na kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2006 ambapo alifunga bao moja kwenye michuano hiyo . Mido pia amewahi kutwaa tuzo za mchezaji bora nchini Ubelgiji ambako alitwaa mara mbili , tuzo ya mchezaji bora wa Misri na tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo barani Afrika mwaka 2001/2002.
Mido amestaafu akiwa amecheza jumla ya mechi 294 kwenye klabu mbalimbali alizopita pamoja na timu za taifa ikiwemo timu ya vijana ambapo amefunga mabao 93 na mpaka anamalizia safari yake ya kucheza soka akiwa  na umri wa miaka 30 huku  klabu yake ya mwisho ikiwa  Barnsley inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England ambayo aliichezea kwenye mechi moja pekee.

0 comments:

Post a Comment