Wednesday, June 5, 2013

Wayne Rooney Aeleza ya Moyoni.



Star wa Manchester United Wayne Rooney amefunguka na kueleza sababu ya kutoelewana na kocha aliyestaafu Sir Alex Fergusson . Rooney amesema kuwa hakupendezwa na kitendo cha kocha huyo kumpanga kwenye nafasi ya kiungo mshambuliaji huku yeye mwenyewe akijiona kama mshambuliaji.

Rooney amesema kuwa anajiona kama mfungaji na anataka kucheza kama mshambuliaji wa kati na hakuridhishwa na kupewa jukumu la kucheza katikati ya uwanja badala ya eneo la 18 la mpinzani ambako atafunga zaidi.
Kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita Wayne Rooney aliripotiwa kuomba kuuzwa kwenye kikao alichofanya na Sir Alex Ferguson ambapo kocha huyo alimwambia kwamba klabu iyo haitamuuuza . Klabu kadhaa ikiwemo Paris St Germain zimekuwa zikitajwa kuwania kumsajili Rooney ambapo matajiri hao wa Ufaransa wameaandaa kitita cha paundi milioni 40 kwa ajili yake.
Hata hivyo kocha mpya wa Man United David Moyes amepanga kumshawishi Rooney kubakia Man United ambapo atafanya mazungumzo na mchezaji huyo atakaporudi toka likizo.

0 comments:

Post a Comment