Wednesday, June 5, 2013

Nigeria wakataa kunywa maji ya Wakenya.


 Barani Afrika mchezo wa soka umetawaliwa na fitna pamoja na mbini chafu ambazo hulenga kumdhoofisha mpinzani hasa kwenye mechi za ugenini ili kutoa faida kwa timu ya  nyumbani kupata ushindi kiwepesi .

Hali hii imedhihirika kwenye maandalizi ya mchezo wa kufuzu kwa kombe la dunia kwa kanda ya Afrika kati ya Nigeria na Kenya ambapo timu ya taifa ya Nigeria imegoma kutumia maji ya kunywa ambayo wamepewa na viongozi wa shirikisho la soka la Kenya ambao kimsingi ni wenyeji wa timu hiyo ya Nigeria .
Kocha wa Mabingwa hao wa Afrika Stephen Keshi alikataa kupokea maboksi 25 ya maji ambayo yaliletwa na kiongozi wa shirikisho la soka la Kenya ambapo alisemakuwa hawahitaji maji hayo na kama wangelazimishwa kuyapokea angewaagiza wachezaji wake wayamwage .
Kitendo hicho kiliwashangaza viongozi wa Fifa waliofika kwenye uwanja wa Kasarani jijini Nairobi ambao walishindwa kuelewa sababu za msingi za kocha huyo kugoma kupokea maji ya kunywa .
Timu ya taifa ya Nigeria inacheza na timu yataifa ya Kenya huko Nairobi baadae hii leo kwenye mchezo muhimu wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2014.

0 comments:

Post a Comment