Wednesday, June 5, 2013

.Usain Bolt kurejea tena baada ya jeraha


Usain Bolt mwanariadha wa Jamaica
Bingwa wa Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za mita mia moja kwa wanaume Usain Bolt wa Jamaica, anatarajiwa kurejea tena uwanja baada ya kuuguza jeraha la mguu, siku ya Alhamisi wakati wa mashindano ya mbio za IAAF Diamond League mjini Rome Italia.

Bolt alipata jeraha hilo la mguu mwezi uliopita na anatarajiwa kushiriki katika mbio za mita mia moja ambapo atapamabana na mshindi wa medali ya shaba katika michezo ya Olimpiki Justin Gatlin.
Mwanariadha wa Uingereza Phillips Idowu ambaye alikosa kushiriki katika michezo ya olimpiki ya London kutokana na jeraha vile vile anarejea tena uwanjani kwa mara nyingine tena.
Idowu atapamba na bingwa wa olimpiki Christian Taylor katika mbio hizo ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali..
Mwaka huu Bolt ameshiriki katika shindano moja pekee la mita mia moja mwezi Mei ambapo alishinda kwa ncha baada ya mshindi kuamuliwa kupitia camera za video, baada ya wanariadha wa kwanza kuonekana kumaliza kwa wakati mmoja na muda sawa wa sekunde kumi nukta sufuri tisa.

0 comments:

Post a Comment