Wednesday, June 5, 2013

EUR0 UNDER 21 KUANZA LEO ENGLAND v ITALY, ISRAEL v NORWAY.


 
2013_UEFA_European_Under-21_Football_Championship
NANI KUTAMBA, ZAHA, STROOTMAN, DZAGOEV, CARVAJAL, KOKE
SPAIN YAWATOA KOMBE LA MABARA ALCANTARA, ISCO & MUNIAIN ILI KUTETEA UBINGWA
YALE MASHINDANO YA UEFA kwa ajili ya Vijana Chipukizi wa chini ya Miaka 21 kuwania Ubingwa wa Ulaya, EURO U-21, yanaanza leo huko Israel kwa Mechi mbili za Kundi A.
Kwa utangulizi, Wenyeji Israel watacheza na Norway na kufuatia England kuivaa Italy.
Mashindano haya ndio chimbuko la Majina makubwa yaliyopata kutokea Barani Ulaya ambao wote walipata kushiriki na hao si wengine bali ni kina Roberto Mancini, Zinedine Zidane, Rudi Voeller, Davor Suker, Luis Figo, Raul na Frank Lampard waliowakilisha Nchi zao.
Mabingwa Watetezi wa Mashindano haya ni Spain waliotwaa Ubingwa Mwaka 2011.
RATIBA:
(SAA za BONGO)
KUNDI A:
Israel v Norway (5 June, Netanya, 19:00)
England v Italy (5 June, Tel Aviv, 21:30)
England v Norway (8 June, Petah Tikva, 19:00)
Italy v Israel (8 June, Tel Aviv, 21:30)
Israel v England ( 11 June, Jerusalem, 19:00)
Norway v Italy (11 June, Tel Aviv, 19:00)
KUNDI B:
Spain v Russia (6 June, Jerusalem, 19:00)
Netherlands v Germany (6 June, Petah Tikva, 21:30)
Netherlands v Russia (9 June, Jerusalem, 19:00)
Germany v Spain (9 June, Netanya, 21:30)
Spain v Netherlands (11 June, Petah Tikva, 19:00)
Russia v Germany (11 June, Netanya, 19:00)
NUSU FAINALI:
Winner Group B v runner-up Group A (15 June, Netanya, 18:30)
Winner Group A v runner-up Group B (15 June, Petah Tikva, 21:30)
FAINALI:
18 June, Jerusalem, 19:00
DONDOO MUHIMU:
-Wachezaji wanaoruhuiwa kushiriki Mashindano haya ni wale waliozaliwa Tarehe 1 Januari 1990 au baada ya hapo.
Kikosi cha England kipo chini ya Kocha Stuart Pearce na kina Wachezaji 23 ambao kati yao ni watano tu ambao hawajachezea Ligi Kuu England.
Lakini Kikosi hicho kitawakosa Nyota Callum McManaman wa Wigan, ambae aling’ara Fainali ya FA CUP walipotwaa Kombe kwa kuifunga Man City Bao 1-0, na pia atakosekana Winga wa Liverpool Raheem Sterling, wote hao wakiwa ni majeruhi.
Katika hao 23 wapo Mchezaji mpya wa Man United, Wilfried Zaha, Viungo wa Liverpool, Jordan Henderson na Jonjo Shelvey, pamoja na Sentahafu wa Tottenham Steven Caulker.
Nao Spain, ili kuhakikisha wanatwaa tena Kombe, wamewachukua Wachezaji Chipukizi wanaochezea Kikosi cha Kwanza cha Mabingwa hao wa Dunia na hivyo kukosa kucheza Kombe la Mabara huko Brazil kuanzia Juni 15, kina Thiago Alcantara wa Barcelona, Mchezaji wa Malaga Isco na yule wa Athletic Bilbao Iker Muniain huku langoni wanae Kipa mahiri wa Man United David De Gea.
WASHINDI WALIOPITA:
2011: Spain
2009: Germany
2007: Netherlands
2006: Netherlands
2004: Italy
2002: Czech Republic
2000: Italy
1998: Spain
1996: Italy
1994: Italy
1992: Italy
1990: USSR
1988: France
1986: Spain
1984: England
1982: England
1980: USSR
1978: Yugoslavia
WACHEZAJI BORA WA MASHINDANO YALIYOPITA:
2011: Juan Mata (Spain)
2009: Marcus Berg (Sweden)
2007: Rosyton Drenthe (Netherlands)
2006: Klaas Jan Huntelaar (Netherlands)
2004: Alberto Gilardino (Italy)
2002: Petr Cech (Czech Rep)
2000: Andrea Pirlo (Italy)
1998: Francesc Arnau (Spain)
1996: Fabio Cannavaro (Italy)
1994: Luis Figo (Portugal)
1992: Renato Buso (Italy)
1990: Davor Suker (Croatia)
1988: Laurent Blanc (France)
1986: Manuel Sanchis (Spain)
1984: Mark Hateley (England)
1982: Rudi Voeller (Germany)
1980: Anatoli Demianenko (USSR)
1978: Vahid Halilhodzic (Yugoslavia)

0 comments:

Post a Comment