Saturday, June 15, 2013

MOYES SAS KAZI KWAKE PAUNI MILIONI 60

Thiago_AlcantaraWAMILIKI wa Manchester United, Familia ya Glazers, wamempa Meneja mpya Davidi Moyes, anaeanza kazi rasmi Julai 1, Pauni Milioni 60 anunue Wachezaji anaowataka yeye mwenyewe ili kumpa uhuru wa kuanza himaya yake na kujenga Timu anayoitaka yeye.
Ila Fedha hizo hazitahusu Uhamisho wa Cristiano Ronaldo endapo Straika huyo wa zamani wa Man United itadhihirika yupo njiani kuihama Real Madrid kama dalili zinavyoonyesha.
Kufuatana na vyanzo vya habari, Pauni hizi Milioni 60 za David Moyes walengwa wake ni Beki wa Everton Leighton Baines, Viungo wa Barcelona Cesc Fabregas na Thiago Alcantara na Straika wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski.DAVID_MOYES-ATUA_MAN_UNITED
Ilitegemewa kundini humo yumo Kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, lakini inaelekea mambo yamepoa hasa baada ya Everton kusisitiza lazima kutimizwa Kipengele cha Mkataba wa Mchezaji huyo cha kulipwa Pauni Milioni 23 ikiwa atahama kabla Mkataba wake kumalizika.
Mwingine anaetazamwa na Moyes ni Gareth Bale wa Tottenham ingawa inaelekea huyo ni ngumu.
Yupo pia Kiungo Mkabaji wa PSV Eindhoven ya Holland, Kevin Strootman, ambae tangu enzi za Sir Alex Ferguson alikuwa akitazamwa sana.
Kwa sasa, Man United inatarajiwa kuwauza Luis Nani na Anderson, na hata Patrick Evra, na mauzo yao yatamwongezea Dau David Moyes kununua Wachezaji wapya ili kuunda Timu anayoitaka yeye.
Dau la Pauni Milioni 60 ni kubwa katika Historia ya Man United ambalo hata Sir Alex Ferguson hajawahi kupewa katika enzi zake zote za Miaka 26 ingawa Msimu uliopita walimnunua Robin van Persie kwa Pauni Milioni 24 toka Arsenal na Shinji Kagawa Pauni Milioni 17 toka Borussia Dortmund na ilibaki kidogo kumsaini Lucas Moura kwa Pauni Milioni 30 kutoka international ya Brazil.
Mwezi Januari, Man United walimsaini Chipukizi toka Crystal Palace, Wilfried Zaha kwa Pauni Milioni 12 huo ukiwa ni Usajili wa mwisho kwa Sir Alex kabla hajastaafu.
                  NI FUNGU KUBWA AMBALO FERGUSON HAJAWAHI KUPEWA!!
                                    HIZO NJE YA  RONALDO IKIWA……!!THESUPERONENEWS.BLOGSPOT.COM

0 comments:

Post a Comment