Wednesday, June 12, 2013

MISS TZ KUTOKA IRINGA 2013 FULL KUJIACHIA



 Washiriki  wa taji la Miss Iringa wakicheza  ngoma na  wasanii  wa Mkwawa Magic Site



















Wakati mashindo  ya  kumsaka Redd's Miss Iringa 2013 yanatarajia  kufanyika siku ya ijumaa katika Ukumbi wa Highlands mjini Iringa ,washiriki  hao  wameendelea  kujinoa kwa  nguvu zote kwa  kufanya mazoezi ya  kufa mtu ili mradi  kila mmoja  kuona ananyakua taji  hilo kwa  mwaka  huu.

Mbali ya  washiriki hao  kila mmoja  kuwa na ndoto ya  kuwa  Redd' S Miss Iringa bado  wametamba  kutwaa taji la Redd's Miss Kanda  ya nyanda  za juu kusini kama  sehemu ya kulivuta  taji la Redd's Miss Tanzania kwa  mwaka huu 2013.

Wakizungumza kwa  majigambo  mengi na mtandao huu  wa www.Thesuperonenews.blogspot.com leo  washiriki hao  wamesema sasa  ni basi  kuona mkoa  wa Iringa  unaendelea  kuwa msindikizaji katika mashindano ya urembo ya  kitaifa na  kuwa lazima kwa mwaka  huu mikoa mingine ikubali taji  hilo kuletwa mkoani Iringa .

Mratibu  wa mashindano hayo mkoani Iringa Dose Maganga alisema  kuwa  jumla ya  washiriki 10  ndio  watao wania taji hilo katika mkoa  wa Iringa.

Amewataja  washiriki hao  kuwa ni Grace Komba (20)elimu ya chuo , Lucy George (19)elimu ya chuo ,Prisca Mengi(19)elimu ya  chuo ,Deborah Jacob (19)kidato  cha  sita ,Neema Mality (18) elimu ya chuo , Lulu Laurent (19)elimu ya  chuo ,Lilian Samson (19) elimu ya  chuo , Frola malya (18) elimu ya  chuo ,Zena Mohamed(20) Kitado  cha nne  na Deborah Samwel(20) elimu ya  chuo

Hata  hivyo alisema  zawadi  kwa mshindi zitatangazwa wakati  wowote kabla ya shindano  hilo  kutokana na kuwepo kwa  dalili za  kuongeza  sehemu ya  zawadi japo hakutaja  zawadi ya  sasa  iliyoandaliwa kwa mshindi.

0 comments:

Post a Comment