Friday, June 7, 2013

KOMBE LA DUNIA 2014:BAADA YA FALCAO KUTIMUKIA MONAKO LEO KUKIPIGA NA MESSI

MESSI_IN_ARGENTINAVINARA wa Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini, Argentina, leo Usiku wanatinga Nyumbani kwao Uwanja wa Klabu ya River Plate, Monumental Stadium Mjini Buenos Aires, kuivaa Colombia katika Mechi ya Mchujo ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil lakini upo wasiwasi mkubwa kama Staa wao Lionel Messi atakuwa fiti kucheza Mechi hiyo muhimu.
Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, amesema wanangoja uthibitisho kama Messi yuko fiti kucheza na Colombia.
Ingawa Messi alijumuishwa kwenye Kikosi cha Argentina kwa ajili ya Mechi zao mbili za Mwezi huu za Mchujo za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia, Mchezaji huyo alizikosa Mechi kadhaa za Klabu yake Barcelona walipokuwa wakimalizia Msimu wao wa La Liga baada ya kusumbuliwa na tatizo la Musuli za Pajani.
Mara baada ya leo Argentina kucheza na Colombia itafuatia Mechi na Ecuador hapo Jumanne.
Akifafanua, Sabella alisema: "Mguu wake uko safi. Anaonekana ni mwepesi na yuko tayari kukabiliana na Mabeki lakini inabidi tuangalie kama yuko fiti baada ya kukaa nje kwa muda mrefu!”
Ikiwa Messi hatacheza, anaweza kubadilishwa na Mchezaji wa AS Roma, Erik Lamela au Walter Montillo wa Klabu ya Brazil, Santos, ambao watatoa sapoti kwa Mastraika wao wa kawaida Sergio Aguero wa Manchester City na Gonzalo Higuain wa Real Madrid.
Argentina wako Pointi 4 mbele ya Ecuador, waliocheza Mechi moja pungufu, na Pointi 5 mbele ya Timu ya 3 Colombia inayoongozwa na Straika hatari Radamel Falcao aliekuwa Atletico Madrid na sasa yuko Monaco ya France.
Colombia wako chini ya Kocha kutoka Argentna, Jose Pekerman, ambae ndie alieipeleka Argentina Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2006.
RATIBA
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Ijumaa Juni 7
23:00 Bolivia v Venezuela [0-1]
Jumamosi Juni 8
01:05 Argentina v Colombia [2-1]
01:10 Paraguay v Chile [0-2]
03:10 Peru v Ecuador [0-2]
Jumanne Juni 11
23:30 Colombia v Peru [1-0]
00:00 Ecuador v Argentina [0-4]
Jumatano Juni 12
01:00 Venezuela v Uruguay [1-1]
01:30 Chile v Bolivia [2-0]
Jumapili Septemba 8
01:00 Colombia v Ecuador [0-1]
01:00 Chile v Venezuela [2-0]
01:00 Paraguay v Bolivia [1-3]
01:00 Peru v Uruguay [2-4]
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Argentina
11
7
3
1
24
8
16
24
2
Ecuador
10
6
2
2
16
10
6
20
3
Colombia
10
6
1
3
19
7
12
19
4
Chile
11
5
0
6
16
19
-3
15
5
Venezuela
11
4
3
4
9
12
-3
15
6
Uruguay
11
3
4
4
17
21
-4
13
7
Peru
10
3
2
5
11
15
-4
11
8
Bolivia
11
2
3
6
13
20
-7
9
9
Paraguay
11
2
2
7
8
21
-13
8
**FAHAMU: Timu 4 za Juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka Kanda ya ASIA kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.

0 comments:

Post a Comment