Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwa Mashujaa Band ambao
waliongoza kwa kuondoka na tuzo nyingi kuliko wasanii wengne. Mashujaa
ambao wanafanya vizuri na wimbo wao wa ''Kidole Risasi'' waliondoka na
kura 5 ikiwa ni pamoja na msanii bora wa kiume band Charz Baba, mtunzi
bora a mashari ya band Charz Baba, rapper bora wa band Furguson, wimbo
bora wa band Risasi Kidole na tuzo ya tano waliichukuwa kupitia category
ya band bora ya mwaka huku wakiwatupa kule Twanga Pepeta, Mapacha
Watatu na Msondo Ngoma
Wakati huo, upande wa hiphop, Kala Jeremiah aliondoka na tuzo tatu na
kuwaacha chini akina Fid Q,Stamina na wengineo, ambapo aliondoka na tuzo
ya msanii bora wa hiphop, mtunzi bora wa mashairi ya hiphop na wimbo
bora wa mwaka ''Dear God''
King Crrazy GK akitoa salam zake baaada ya kupigiwa shangwe la hatari alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya mssanii bora wa Hiphop
Ommy Dimpoz nae, alisepa na tuzo tatu , wimbo bora wa kushirikiana ''me
and you'', video bora ya mwaka ''Baadae'' na wimbo bora wa bongo pop
kutoka arusha, Jambo Squad waliwakilisha vizuri baada ya kuchukua tuzo ya kundi bora la muziki wa kizazi kipya
Mrisho Mpoto ameondoka na tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili ''chocheeni kuni''
mtayarishaji boa wa mwaka ni Man Walter
Ben pol aliondoka n tuzo ya mtunzi bora wa muziki bongo fle
va
wengine ni pamoja na Diamond ambae aliondoka na tuzo ya msanii bora wa
kiume na msanii bora wa kiumee bongo fleva. msanii anaechipukia ''Ally
Nipishe'', mtayarishaji anaechipukia ''Mensen Selector, wimbo bora wa
hiphop ''nasema nao'' Ney wa mitego, wimbo bora wa Zouk/Rhumba ''ni
wewe'' Amini, wimbo bora wa Africa mashariki ''Valu valu'' Chameleon,
msanii bora wa kike ''Jay Dee,
0 comments:
Post a Comment