Thursday, June 6, 2013

LISTI YA FUFA UBORA DUNIANI YATOKA 4 BORA ZILE ZILE, BONGO YAPANDA NA

FIFA_LOGO_BESTKATIKA Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa leo, Mabingwa wa Dunia Spain bado Nambari Wani wakifuatiwa na Timu zile zile 3 toka Mwezi uliopita, yaani Germany, Argentina na Croatia, huku Tanzania ikipanda Nafasi 7 kutoka 116 hadi 109.
Katika 10 Bora, Netherlands imechupa hadi Nafasi ya 5, Portugal kushuka Nafasi moja hadi ya 6, Colombia, wameshuka Nafasi 2 na wapo wa 7 na England wameporomoka Nafasi 2 na sasa wako Nafasi ya 9.
Kwa Nchi za Afrika, Côte d'Ivoire ndio ipo Nafasi ya juu kabisa ikiwa Nafasi ya 13 ikifuatiwa na Ghana iliyo Nafasi ya 20.
Brazil, ambayo imeathirika kwa kucheza Mechi za Kirafiki tu kwa Miaka miwili, imeporomoka Nafasi 2 na sasa ipo Nafasi ya 22 lakini kushiriki kwao katika Mashindano rasmi ya FIFA ya kugombea Kombe la Mabara yatakayochezwa Nchini kwao kuanzia Juni 15, ikiwa watafanya vizuri, kutawasaidia sana kupanda chati.
Toleo jingine la Listi ya FIFA ya Ubora Duniani litatolewa Julai 4.
25 BORA:
1        Spain
2        Germany
3        Argentina
4        Croatia
5        Netherlands
6        Portugal
7        Colombia
8        Italy
9        England
10      Ecuador
11      Russia
12      Belgium
13      Côte d'Ivoire
14      Switzerland
15      Bosnia-Herzegovina
16      Greece
17      Mexico
18      France
19      Uruguay
20      Denmark
21      Ghana
22      Brazil
23      Mali
24      Czech Republic
25      Chile
NCHI ZINAZOIZUNGUKA TANZANIA:
104    Qatar
105    Lithuania
106    Ethiopia
107    Niger
108    Saudi Arabia
109    Malawi
109    Tanzania [IMEPANDA NAFASI 7]
111    Kuwait
112    Tajikistan
113    Suriname
114    Korea DPR
115    Benin 308
116    Northern Ireland

0 comments:

Post a Comment