Tuesday, June 11, 2013

“Kama Barca wakinifukuza nitaondoka” Kauli ya Cesc Fabregas.




“Kama Barca wakinifukuza nitaondoka” Kauli ya Cesc Fabregas.
Star wa Fc Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Francesc ‘CESC’ Fabregas amezungumzia tetesi zilisombaa juu ya mustakabalia wa maisha yake ndani ya Barca   kuwa ataendelea kubaki mchezaji wa Barcelona hadi hapo klabu hiyo itakapoamua vinginevyo. Cesc kwa maneno yake amesema kuwa “Kama Barcelona wakisema kuwa hawanihitaj.

Hayo yatakuwa mengine -ila ninachotaka kwa sasa ni kuendelea kupata mafanikio ndani ya klabu hii na si kinyume na hapo ” . Fabregas aliendelea kusema kuwa ametokea mbali na klabu hiyo na hafikirii kutupa historia yote aliyonayo ndani ya Barca kwa kwenda mahali kwingine .
Cesc Fabregas amehusishwa na usajili wa klabu ya Manchester United ambayo kocha wake David Moyes ametajwa kuandaa paundi milioni 40 za kumsajili kiungo huyo .
Baadhi ya mashabiki wa Barcelona wamekuwa wakimshutumu mchezaji huyo kwa kutokuwa na mwendelezo mzuri kwenye kiwango chake hasa kwa msimuu huu uliopita jambo ambalo linaweza kuwa sababu ya tetesi hizo .
Hata hivyo mchezaji huyo ambaye kimsingi Barcelona ni nyumbani kwao ametoka na kukanusha taarifa zilizopo japo tetesi nyingine zimekuwa zikisema kuwa Uongozi wa Barca uko tayari kusikiliza ofa zote zitakazokuja kwao kwa ajili ya Fabregas kwani mchezaji huyo ameshindwa kufikia malengo ambayo klabu hiyo ilikuwa nayo kwake wakati ikimsajili toka Arsenal .
Fabregas kwa sasa yuko nchini Brazil akiwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambacho kinashiriki michuano ya kombe la mabara inayotarajiwa kuanza wikiendi ijayo.                                                                                                                                                             

0 comments:

Post a Comment