Saturday, June 15, 2013

KAGAME CUP: SERIKALI YARUHUSU USHIRIKI WAKATI YANGA, SIMBA KAMBI ZISHAVUNJWA!

KAGAME_CUP_2012USHIRIKI wa Timu za Tanzania kwenye Mashindano ya CECAFA ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, KAGAME CUP yaliyokuwa yaanze Juni 18, umeingia kwenye utata mkubwa kufuatia Klabu za Yanga na Simba kuvunja Kambi zao.
 kutokana na kuhofia usalama wao huko Darfur, Sudan lakini Jana Serikali ya Tanzania ilipokea uthibitisho wa usalama wa Timu kutoka Serikali ya Sudan na wao kutoa ruksa kwa Timu kushiriki.
Akiongea huko Dodoma hiyo Jana, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, alisema Serikali imepata uthibitisho toka Serikali ya Sudan kwamba Timu za Tanzania zitapewa ulinzi wa kutosha na kuhakikisha usalama wao.
Tanzania ilikuwa iwakilishwe na Timu 3, Yanga, kama Mabingwa Watetezi wa Kagame Cup, Simba kama Mabingwa Tanzania Bara Msimu wa 2011/12 na Falcon FC ya Zanzibar kama Mabingwa wa Zanzibar Msimu uliopita.
Hata hivyo, hadi sasa haijulikani kama Timu hizo zitashiriki, hasa Yanga na Simba, ambazo mara baada ya kuambiwa na Serikali kwamba huko Darfur hamna uhakika wa usalama wao, Timu hizo zilivunja Kambi za Mazoezi na kuwapa Likizo Wachezaji wao.
Mbali ya Timu za Tanzania kujitoa, Tusker FC ya Kenya pia ilijitoa ikihofia usalama wake.
Vile vile, hiyo Jana Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, alishatangaza kubadilisha Ratiba na kuziingiza Electric Sports ya Chad [Si Mwanachama wa CECAFA] na URA ya Uganda.
Timu ambazo zimebaki kushiriki Mashindano hayo ni:  Al Ahly Shandi (Sudan), Al Nasir (South Sudan), Al-Hilal Kadugli (Sudan), Express FC (Uganda), URA FC (Uganda), Ports FC (Djibouti), Vital’O  (Burundi), Merriekh El Fasher (Sudan), APR (Rwanda), Elman (Somalia), Rayon Sport  (Rwanda) na Electric Sport (Chad). 
TUSKER YA KENYA ILISHAJITOA KUHOFIA USALAMAThesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment