Wednesday, June 5, 2013

JOSÉ MOURINHO ADAI RONALDO ANAJIDAI KUJUA KILA KITU!

 
RONALDO_MWANAMUZIKIMENEJA MPYA wa Chelsea, Jose Mourinho, ameungama kuwa licha ya kuwa na Misimu mitatu mizuri pamoja walipokuwa na Real Madrid, tatizo lake pekee na Supastaa Cristiano Ronaldo ni kwamba anadhani Mreno huyo mwenzake ana tabia ya kujiona anajua kila kitu.
Ronaldo, ambae alijiunga na Real Mwaka 2009 kwa Dau la Pauni Milioni 80 lililomfanya awe Mchezaji wa bei ghali kupita wote Duniani, akiwa na Real chini ya Mourinho alizidisha kasi yake ya ufungaji Bao nyingi.
Akihojiwa na kwenye Shoo ya TV, Punto Pelota, huko Spain, Mourinho, ambae ataanuliwa rasmi kuwa Meneja mpya wa Chelsea Jumatatu ijayo, akielezea jinsi uhusiano wake na Ronaldo ulivyoyumba Msimu uliopita, alinena: “Nilikuwa na tatizo moja tu na Ronaldo. Tatizo dogo na rahisi tu ambalo Kocha akimlaumu Mchezaji ili kuboresha mbinu za Timu, Mchezaji huchukia. Wakati huo alikuwa hakubaliani na hilo labda kwa vile anajiona anajua kila kitu na Kocha hawezi kumuendeleza chochote!”
Mourinho aliongeza: “Cristiano alikuwa na Misimu mitatu mizuri na mimi. Sijui kama ilikuwa ndio bora kwake kwani akiwa na Manchester United alipata mafanikio makubwa! Lakini nadhani, kimbinu, tulimtengenezea hali nzuri ya kumfanya atumie kipaji chake kuweka rekodi na kufunga Bao nyingi!”
Baada kuondoka Mourinho, zipo tetesi nzito kuwa nae Ronaldo anataka kuondoka Real huku Man United ikitajwa sana pamoja na Chelsea.
Hata hivyo, Rais wa Real, Florentino Pérez, hivi Juzi alisisitiza Ronaldo haendi popote.

0 comments:

Post a Comment