Friday, June 7, 2013

JAPHET KASEBA AJIPANGA NA MMALAWI KESHO DDC MAGOMENI KONDOA LEO WAPIMA UZITO



Bondia Japhet Kaseba leo amepima tayari kumkabili mpinzani wake Rasco Chimwanza wa Malawi katika pambano la ubingwa wa kimataifa.
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony Ruta, Ibrahim Kamwe, Pendo Njau na Dr. John Lugambila wa Muhimbili na kueleza kuwa mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani.
 
Kaseba amejinadi kumsambaratisha mpinzani wake katika raundi za mapema za mchezo huo. Pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kama Juma Fundi atazipiga na Hasan Kiwale (moro best), Joseph Onyango toka Kenya atazipiga na Seba Temba wa Morogoro, huku Issa Omar Peche boy atakapomvaa bondia mkongwe Juma Seleman na mapambano mengineyo mengi yatapigwa katika ukumbi huo wa DDC Magomeni Kondoa 

0 comments:

Post a Comment