Wednesday, June 5, 2013

Harambee Stars ya Kenya yaambulia patupu

Nigeria wanasemekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda mechi ya leo
Harambee Stars imeondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kombe la dunia 2014

Mchuano wa kufa na kupona ulishuhudiwa kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi.
Musa Ahmed aifungia Nigeria bao la kwanza na la pekee kunako dakika ya 81. Mashabiki wa Kenya Kimya!
Baadhi ya mashabiki wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars waanza kuondoka uwanjani.
Mashabiki wa Nigeria hawakuwa wengi uwanjani wakikisiwa kufika 300, lakini licha ya uchache wao ,hawakufa moyo.Mandishi wa BBC Odeo Sirari aliyekuwa uwanjani,alishuhudia mashabiki wachache wa Nigeria wakiisiahngilia timu yao kwa nyimbo na ngoma japo hawakuwa wanasikika kutokana na mayowe ya wakenya.
Ilikuwa mechi ya mkondo wa pili kwa timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja walipocheza kwa mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana.
Mechi hii ni ya kundi la F ya kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Vijana wa kocha Stephen Keshi, wanatarajiwa kuendeleza ushindi wao hii leo wakijitafutia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michauno ya kombe la dunia nchini Brazil
Kwa vijana wa Eagles wanaosemekana kujiandaa vyema, wanafahamu kuwa ikiwa watashindwa basi itakuwa hasara kwao kwani hawataweza kwenda Brazil.
Licha ya kwenda sare mwezi jana, Nigeria inaingia kwenye mkondo huu bila ya kushindwa mechi yoyote ya makundi kati ya kumi na sita zilizocheza hadi kufikia sasa.

Timu zote zina mbili zina uhakika zitashinda mechi ya leo. Tuache tuone msema kweli
Mechi inatarajiwa kuanza saa kumi kamili. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria
 Mashabiki washangilia wachezaji wa Harambe Starrs wakiingia uwanjani. Super Eagles nao pia  Kikosi cha Harambe Stars: Mlinda lango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David Owino Brian Mandela David Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto, Victor Wanyama Jamal Mohammed,Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa Aswani na Fracis Kahata
Mechi imeng'oa nanga rasmi .na  Kikosi cha Eagles...Efe, Oboabona, Omeroo Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa, Ideye Golikipa ni Enyeama Mshambuliaji wa Kenya Kepha Aswani anenekana akichechema uwanjani na kuwa mashabiki wanataka aondolewe

 
 Opiyp atekeleza shambulizi lango la Nigeria.
lakini pia Nigeria yafanya mabadiliko, SundayMba aondolewa
pia Victor Wanyama apata jeraha..anahudumiwa. Kenya yashambulia, Kombora la Johhana Ngeno lapaja juu ya mlingoti kunako dakika ya 56. Victor Wanyama arejea uwanjani, mashabiki wa kenya washangilia. Nigeria inahitaji ushindi katika mechi hii dhidi ya Kenya ili kusonga mbele. Sare ya kutofungana itaipa Kenya nafasi nzuri ya kusonga mbele
 Mlinzi wa kati wa Harambee Stars Brian Mandela amefanya kazi ya ziada kupangua makombora ya wa Nigeria.
Mashabiki wa Kenya wanaimba: '' Haki yetu! Bao! Haki yetu! bao!
Timu ya taifa ya Nigeria yafanya mabadiliko dakika ya 64 anaondoka Brown Aye anaingia Ujah Antony
Victor Wanyama arejea tena uwanjani licha ya kuonekana amejeruhiwa. Mashabiki wa Kenya wakiwanataka aendelee kucheza.
 Mulinge Munandi aonyeshwe kadi ya njano kwa kumfanyia masihara mchezaji wa Nigeria Musa Ahmed. Harambee stars yazidisha shinikizo dhidi ya Super Eagles. Mashabiki wakosa subira.. wanaimba haki yetu! bao! haki yetu! bao.....
Peter Opiyo wa harambee stars aondolewa, Patrick Osiakonaye alipata nafasi ya kuaingia uwanjani.
 Mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria kama mia 200 hivi walishangilia bao lililofungwa na Musa Ahmed. Baadhi ya mashabiki wa Kenya wawazomea wenzao wa Nigeria kwa kuwarushia chupa za maji.
Safu ya mashambulizi ya Harambee stars yaonekana kufifia.
Dakika ya 87, Oduamani wa Nigeria aondoka anaingia Ogude.
Nigeria yapata kona ya pili kipindi cha lala salama.

0 comments:

Post a Comment