Friday, June 7, 2013

FERNANDINHO YUKO CITY, HULK ATHIBITISHA CHELSEA, FELLAINI….ARSENAL

FERNANDINHOZILE NYAKATI za vikumbo vya Uhamisho wa Wachezaji kabla Msimu mpya kuanza ndio zimepamba moto na Manchester City tayari wameshamnasa Staa wa Brazil Fernandinho huku Staa mwingine wa Nchi hiyo, Hulk, akithibitisha Chelsea kumuwania wakati huko Etihad zipo habari za Arsenal kumtaka Kiungo wa Everton Marouane Fellaini.
HULK
Straika wa Klabu ya Urusi Zenit St Petersburg, Hulk, ambae kwa sasa yuko na Kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kinachojitayarisha kwa ajili ya Mashindano ya Fifa ya kombe la kagame la mabala yatakayochezwa huko Brazil kuanzia Juni 15, amebainisha kuwa Chelsea inataka kumsaini.
Hulk, alipohojiwa, alijibu: “Nikisema kuwa hamna lolote, nitakuwa nadanganya! Lakini haya si kwa sasa. Kwa sasa nipo Aslimia 100 na Brazil na nategemea kushinda Kombe la Mabara! Mengine yatasubiri hadi baadae!”
FELLAINI
Huko London, upo uvumi mzito kuwa Kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, huenda akachukuliwa na Arsenal ambao inadaiwa wako tayari kulipa Pauni Milioni 24 ambalo ndio Dau lililopo kwenye Mkataba wa Mbelgiji huyo ikiwa anataka kuvunja Mkataba na Everton.
Ingawa imedaiwa sana kuwa Fellaini atamfuata aliekuwa Meneja wake huko Everton, David Moyes, ambae sasa yupo Manchester United, lakini uvumi huo wa Kiungo huyo kwenda Arsenal unadai kuwa Old Trafford inasita kumchukua hasa kwa sababu ya staili yake ya uchezaji iko tofauti na ile ya Klabu hiyo ingawa pia hilo hilo linaweza kusemwa kwa staili ya Arsenal.
CITY YAMSAINI FERNANDINHO
Manchester City imekamilisha kumsaini Kiungo wa Klabu ya Ukraine Shakhtar Donetsk, Fernandinho, kwa kitita cha Pauni Milioni 30.
Fernandinho, mwenye Miaka 28 na ambae ameichezea Brazil mara 5, amesaini Mkataba wa Miaka minne.
Fernandinho anakuwa Mchezaji wa kwanza kusainiwa na Man City katika Kipindi hiki ingawa pia wana makubaliano ya kumchukua Winga wa Sevilla ya Spain, Jesus Navas.
Hadi sasa, Man City haina Meneja baada ya kutimuliwa Roberto Mancini mwishoni mwa Msimu ulioisha Mei lakini inatarajiwa Wiki ijayo Meneja wa Klabu ya Spain Malaga, Manuel Pellegrini, atatangazwa rasmi kuwa Meneja wao mpya.
FERNANDINHO:
-Jina kamili: Fernando Luis Roza
-Klabu: Atletico Paranaense (2002-2005); Shakhtar Donetsk (2005-2013)
-Mechi: 385
-Magoli: 68
-Brazil: Mechi 5
Akiongelea Uhamisho wake, ambae inadaiwa alisamehe Pauni Milioni 4 za Mkataba wake na Shakhtar Donetsk ili ahamie Man City, alisema: “Lengo langu hapa ni kutwaa Ubingwa! Hapa ipo Timu imara, Klabu bora na Mashabiki ni wazuri! Kuchezea Klabu kubwa katika Ligi kubwa kutanipa furaha! Nitalipa fadhila!”

0 comments:

Post a Comment