Saturday, June 15, 2013

FAHAMU KILICHHO SABABISHA MLIPPUKO WA BOMU ULIOTOKEA JIJINI ARUSHA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA


Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu waliojitolea wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.

 
Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.



Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA. Mwandishi mmoja wa habari anaripotiwa kunyang’anywa kamera yake baada kwa kupiga picha, hata baada ya kujitambulisha.
Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano huo waCHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni zauchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.WWW.THESUPERONENEWS.BLOGSPOT.COM

0 comments:

Post a Comment