EVERTON KULIPA FIDIA YA KUMCHUKUA MARTINEZ KWA WIGAN
Everton wamefikia makubaliano na Wigan ya kuwalipa fidia ikiwa watamchukua Meneja wao Roberto Martinez.
Martinez, Raia wa Spain mwenye Miaka 39,
anatarajiwa kumbadili David Moyes ambae anahamia Manchester United
kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson aliestaafu.
WASIFU: Roberto Martinez
MIAKA: 39
UCHEZAJI: Real Zaragoza
(1993-94), Balaguer (1994-95), Wigan Athletic (1995-2001), Motherwell
(2001-02), Walsall (2002-03), Swansea (2003-06), Chester City (2006-07).
MATAJI KAMA MCHEZAJI: Copa del Rey (1994), Football League Third Division (1997), Football League Trophy (1999 & 2006)
UMENEJA: Swansea (2007-09) na Wigan Athletic (2009-13).
MATAJI KAMA MENEJA: Football League One (2008) & FA Cup (2013).
Inatarajiwa kuhamia kwa Martinez kwenda Everton kunaweza kuthibitishwa katika Masaa 48 yajayo.
Msimu huu Martinez aliiwezesha Wigan
kutwaa Kombe la FA CUP walipoifunga Manchester City Bao 1-0 lakini Siku
chache baadae wakaporomoka Daraja toka BPL, Barclays Premier League na
Msimu ujao watacheza Daraja la chini, Championship.
MAN CITY YAMCHUKUA WINGA WA SEVILLA JESUS NAVAS
Manchester City wamefikia makubaliano na Klabu ya Spain Sevilla ya kumnunua Winga wa Kimataifa wa Spain Jesus Navas.
Navas, mwenye Miaka 27, anategemewa kununuliwa kwa gharama ya Pauni Milioni 17.
Navas yumo kwenye Kikosi cha Spain kitakachocheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara huko Brazil kuanzia Juni 15.
Hadi sasa Man City haijatangaza nani
Meneja wao mpya baada ya kumtimua Roberto Mancini ingawa wengi
wanategemea Manuel Pellegrini, aliekuwa Malaga, ndio atachukua nafasi
hiyo.
JOSE MOURINHO: “KURUDI TENA CHELSEA NI KAZI RAHISI KWA SABABU NI NYUMBANAI KWAKE.
Mara baada ya Chelsea kuthibitisha kuwa
Jose Mourinho ndie atakuwa Meneja wao mpya, hii ikiwa ni mara ya pili
kwa yeye kushika wadhifa huo baada ya kuwa hapo kati ya Miaka 2004 hadi
2007, Mourinho ametamka kuwa uamuzi wa kurudi kwake ulikuwa rahisi.
Mourinho alisema: “Nilimuuliza Bosi
[Abramovich] unataka nirudi? Na yeye akaniuliza, unataka kurudi? Baada
ya Dakika chache uamuzi ukafanywa!”
Akigusia mipango yake na Chelsea,
Mourinho aligusia kuwa nia yake ni kuiboresha Timu lakini si kwa kutumia
Mamilioni kuwanunua Wachezaji wapya.
Msimu huu uliopita Chelsea ilimaliza BPL ikiwa Nafasi ya 3 na pia kutwaa Kombe la EUROPA LIGI
0 comments:
Post a Comment