Tuesday, June 4, 2013

BOBAN AJIUNGA RASMI NA COASTAL UNION.


Hatimae kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba Haruna Moshi 'Boban' amesajiliwa rasmi na Coastal Union ya mkoani Tanga,Boban ambaye hivi karibuni alitangazwa kuachwa na klabu yake ya zamani Simba SC amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwachezea 'wagosi wa kaya'.
Haruna Moshi aliwahi kuichezea Coastal Union mnamo mwaka 2000 ambapo alidumu hapo kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Moro UTD mnamo mwaka 2001. 
 Boban akisaini mkataba wa kujiunga na Coastal Union.
Boban akiwa ndani ya jezi ya Coastal Union akisalimiana na Kocha wa timu hiyo Hemed Moroko.

0 comments:

Post a Comment