Thursday, June 13, 2013

Barcelona yaingia kwenye mbio za kumsaini Torres pamoja na David luiz

Fernando-Torres-Chelsea-Europe-League-2013-HD-Wallpaper Fc Barcelona wameingia rasmi kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres
ambaye anaonekana kutokuwa chaguo la kocha mpya wa klabu hiyo Jose Mourinho . Kwa mujibu wa gazeti la The Sun , Barca wameandaa kitita cha paundi milioni 17 kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye Chelsea ilimnunu akwa paundi milioni 50 toka Liverpool.

Maisha ya Torres ndani ya Chelsea yamekuwa magumu tangu alipoingia kwenye klabu hiyo na kauli ya kocha Mourinho kumtaja mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku kuwa ataongoza mashambulizi ya Chelsea msimu ujao imekuwa kama ishara kwa Torres kuanza kuchukua kila kilicho chake na kutafuta pa kwenda.
Barcelona wanatafuta mshambuliaji ambaye ataipa safu ya ushambuliaji taswira tofauti na ile iliyozoeleka ikiongozwa na Lionel Messi . Hata hivyo Torres ni mmoja wa wachezaji wanaopendwa na mmiliki wa klabu hiyo Bilionea wa Urusi Roman Abramovich na hiyo inaweza kuwa sababu ambayo huenda ikamfanya abakie na Chelsea.
Msimu uliopita ulikuwa msimu bora kwa Torres tangu ahamie Chelsea ambapo alifunga mabao 21 kwenye mashindano yote yakiwemo mabao muhimu kama kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Benfica . Hata hivyo Mourinho havutiwi na aina ya uchezaji wa washambuliaji kama Torres na amekuwa sokoni akisaka kuwanunua washambuliaji kama Edinson Cvanni ambye jina la Torres limehusishwa na mabadilishano ya mchezaji huyo kwenda klabu ya Napoli anakotoka Cavanni na Hulk wa Zenith St Petersburg. Barca pia wamehusishwa na tetesi za usajili wa beki wa kimataifa wa Brazil David Luiz ambaye kama ilivyo Torres sio chaguo la kwanza kwa Mourinho.                                                                                   
  david luiz

0 comments:

Post a Comment