Friday, June 7, 2013

Bayern Munich yauza tiketi zote za mechi za nyumbani kwa msimu ujao.




bayern bavaria Waswahili wana msemo usemao kuwa “Biashara Asubuhi,Jioni Mahesabu”,Mabingwa wa Ujerumani na Ulaya Bayern Munich wanaonekana kukubali msemo huu kwa asilimia mia moja baada ya kufanikiwa kuuza tiketi zote za mechi za nyumbani kwa ajili ya msimu ujaao wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga .

Bayern Munich wameuza tiketi za mechi 16 za uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena huku ukisalia mchezo mmoja pekee ambao tiketi zake hazijauzwa  na yote haya yamefanyika zikiwa zimebaki wiki tisa kabla ya msimu mpya wa Bundesliga kuanza huku ratiba ya michezo hiyo  ikiwa bado haijatoka .
Munich wanasifika kwa kuingiza fedha yningi kutokana na mauzo ya tiketi za michezo yake pamoja na vyanzo vingine mbalimbali na kwa msimu huu uliopita walifanikiwa kuipiku Manchester United kama klabu ya soka yenye thamni kuliko zote barani ulaya .
Munich wana kawaida ya kumaliza mauzo ya tiketi za mechi zao za uwanja wa nyumbani mapema na msimu uliopita walifanya hivyo mpaka kufikia Julai 11 rekodi ambayo wameivunja kwa mwezi mmoja safari hii.
Ligi ya Bundesliga inasifika kwa kuwa na tiketi zenye gharama ndogo tofauti na ligi nyingine barani ulaya kama Ya England ambapo tiketi ya Mchezo mmoja kwenye uwanja wa Emirates ambayo gharama yake ni euro 92 inaweza kutosha kuingia uwanjani kwenye mechi zote 17 za nyumbani kwenye uwanja wa Allianz Arena , na ni kwa sababu hii mechi za Bundesliga hujaza mashabiki kuliko mechi zote za ligi barani ulaya .

0 comments:

Post a Comment