Friday, June 14, 2013

UBORA WA LIGI KUU ENGLAND WAONEKANA!!!

CHICHA_ANAUMIZWA12
NDIO LIGI YENYE RAFU CHACHE UKILINGANISHA NA LIGI VIGOGO ULAYA!
WASIMAMIZI wa Ligi Kuu England, BPL, Barclays Premier League, wametoa Takwimu ambazo zinaonyesha Rafu kwenye Mechi za Ligi hiyo zimepungua kwa Asilimia 22 tangu Mwaka 2006.
Akiongelea mwenendo huo, Mkuu wa Mrefa, Mike Riley, amesema: “Frikiki zimepungua polepole na kuifanya Gemu iwe ya haraka na mtiriko zaidi na kuifanya ivutie na kupendeza!”
Katika Msimu wa 2012/13 kwenye Mechi 380 za Ligi Kuu Rafu 8,562 zilifanyika ikiwa ni sawa na wastani wa Rafu 22.5 kwa kila Mechi.
Riley amedokeza Takwimu hizo zinaonyesha kuwa England ina Rafu chache ukilinganisha na Ligi nyingine kubwa Barani Ulaya.
NCHI
LIGI
RAFU KWA GEMU
England
LIGI KUU
23
Spain
LA LIGA
29
France
LIGI 1
31
Italy
SERIA A
31
Germany
BUNDESLIGA
32
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kwenye Ligi Kuu, katika Msimu wa 2005/06, Rafu 10,886 zilifanyika ukiwa ni Wastani wa Rafu 28.6 kwa Mechi.
Hata hivyo, Msimu uliopita Mameneja kadhaa walilalamikia kuhusu Mchezo wa nguvu na Rafu na hao ni pamoja na Wakongwe Arsene Wenger na Sir Alex Ferguson.
Kwenye Mechi iliyochezwa Emirates Mwezi Aprili kati ya Arsenal na Everton, Wenger alilalamika kwamba Refa Neil Swarbrick aliacha Rafu nyingi bila kutoa adhabu.
Nae Meneja Mstaafu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aliwahi kulalamika kuhusu Straika wa West Ham, Andy Carroll kumvaa Kipa wao David De Gea na kudai Straika huyo alipaswa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
KEVIN DAVIES:
-Kevin Davies: Katika Misimu 7 kati ya 9 iliyopita Mchezaji huyu wa Bolton Wanderers ndie aliecheza Faulo nyingi kupita yeyote.
-Kevin Davies: Katika Misimu ya 2005/06 na 2008/09 ndie Mchezaji aliechezewa Faulo nyingi kupita yeyote.
Pia Msimu uliopita wa 2012/13 ulikuwa na Kadi Nyekundu chache katika Miaka 16 kwa Kadi 52 kutolewa, sawa na Msimu wa 2006/7, lakini Kadi chache kabisa kutolewa ni 1996/7 zilipotoka 44.
Msimu wa 2011/12 zilitoka Kadi Nyekundu 66 na Rekodi inashikiliwa Msimu wa 2005/6 zilipotolewa Kadi Nyekundu 73.
Kushuka kwa Takwimu hizi kunadaiwa ni kwa sababu ya Elimu wanayopewa Wachezaji na Maafisa toka Bodi ya Marefa na pia Wachezaji hao kupata mwamko kuhusu usalama wa wenzao.
FAULO KATIKA MECHI ZA LIGI:
MSIMU
MECHI
FAULO JUMLA
FAULO KWA MECHI
2012-13
380
8562
22.5
2011-12
380
8307
21.9
2010-11
380
9215
24.3
2009-10
380
9986
26.3
2008-09
380
9647
25.4
2007-08
380
10066
26.5
2006-07
380
10415
27.4
2005-06
380
10866
28.6
Takwimu na Opta
Nae Mchezaji mtukutu kupita wote, Kevin Davies wa Bolton Wanderers, anaamini Rafu na matukio kwenye Mechi yatapungua sana ikiwa Marefa watafanya kazi pamoja na Makeptini wa Timu zinazocheza.
Davies amedai Marefa wanapaswa kuwasisitiza Makeptini waongee na Wachezaji wao wakorofi ili kupunguza munkari na kujichunga.TThesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment