CEO wa klabu ya Sunderland, Margaret Byrne, ameusifia ushirikiano na Tanzania kwamba ni hatua kubwa kuendelea mbele.
The
Black Cats wameingia mkataba na kampuni ya nishati ya Power kujenga
cademy kubwa ya soka nchini, ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Raisi
Jakaya Kikwete alitembelea makao makuu ya klabu ya Sunderland huko
Wearside siku ya jumapili katika kukata rasmi utepe wa kuanza kwa
project hiyo.
“Ni siku muhimu kwa klabu na klabu na mji wetu,” Byrne alisema.
“Kutembelewa
na mheshimiwa Raisi hapa wakati akiwa UK kuhudhuria mkutano wa viongozi
wa G8 ni jambo kubwa kutoka kwake na mawaziri wake. Ni zuri sana kwetu.”
Hatua
za mwanzo kwa ajili ya Academy zilizinduliwa siku hiyo ya jumapili,
kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na mwenyekiti wa Sunderland Ellis
Short.
Project
hiyo itaisaidia Tanzania katika kukuza soka lake pia kuwapa nafasi
kubwa vijana wadogo kabisa kuweza kuendeleza vipaji vyao kwenye academy
hiyo.
Sunderland watajenga majengo pamoja na kutoa makocha wa kufundisha.
“Hatua
ya kwanza itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion Power kujenga
academy ya kijamii, tukiruhusu watoto wengi kuja na kufurahia kucheza
mchezo wa soka,” Byrne alielezea.
“Hatua
ya pili itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion labda ikiwezekana na
taasisi nyingine kujenga kituo cha kisasa cha kufundishia soka.
“Tutoa
usaidizi mkubwa wa vifaa vingi tunavyotumia kwenye academy yetu ya
Academy of Light na pia na maarifa tuliyoyapata na tunayoyapata kutoka
kwenye project ya EPPP (Elite Player Performance Plan).Www.Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment