Sunday, June 9, 2013

FIFA KOMBE LA MABARA: NIGERIA WAJIPANGA UPYA KWA KUTOA DOZI I!

STEPHEN_KESHIMABINGWA wa AFRIKA, Nigeria, wametangaza Kikosi chao kitakachosafiri kwenda Brazil kushiriki Mashin dano ya FIFA ya kombe la mabra yatakayoanza Juni 15 na kuna mabadiliko 9 katika Kikosi kilichotangazwa na Kocha Stephen Keshi toka kile kilichotwaa AFCON 2013.

Kabla kwenda huko Brazil ambako wamepangwa KUNDI B la Kombe la Mabara pamoja na Spain, Uruguay na Tahiti, Nigeria watasafiri kwenda huko Mjini Windhoek kucheza na Namibia hapo Jumatano kwenye Mechi ya KUNDI F la Bara la Afrika kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
KUNDI A la Kombe la Mabara lina Timu za Brazil, Japan, Mexico na Italy.
Wachezaji walioachwa wa Nigeria ni pamoja na Victor Moses, Emmanuel Emenike, Joseph Yobo, Peter Odemwingie na Obafemi Martins.
Miongoni mwa Wachezaji walioteuliwa kwa safari ya Brazil wapo Wachezaji wanne ambao ni mara yao ya kwanza kuitwa.
Katika KUNDI F la Bara la Afrika kwa Mchujo wa Kombe la Dunia, Nigeria ndio Vinara wakiwa Pointi 2 mbele ya Malawi, wakifuata Namibia na mkiani wapo Kenya.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Chigozie Agbim (Enugu Rangers), Austin Ejide (Hapoel Beer Sheva), Vincent Enyeama (Maccabi Tel Aviv)
MABEKI: Efe Ambrose (Celtic), Francis Benjamin (Heartland FC), Elderson Echiejile (Sporting Braga), Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves), Solomon Kwambe, Godfrey Oboabona (both Sunshine Stars), Kenneth Omeruo (ADO Den Haag)
VIUNGO: Emeka Eze (Enugu Rangers), John Obi Mikel (Chelsea), Fegor Ogude (Valerenga), John Ogu (Academica Coimbra), Ogenyi Onazi (Lazio), Sunday Mba (Enugu Rangers)
MAFOWADI: Joseph Akpala (Werder Bremen), Michael Babatunde (FC Kryvbas), Muhammad Gambo (Kano Pillars), Brown Ideye (Dynamo Kiev), Ahmed Musa (CSKA Moscow), Nnamdi Oduamadi (Varese), Anthony Ujah (FC Cologne).

0 comments:

Post a Comment