Tuesday, June 4, 2013

Bingwa wa Olimpiki abwagwa Marekani

Ezekiel Kemboi
Mwanariadha wa Burundi Francine Niyonsaba, aliandikisha ushindi wake wake kwanza katika mashindano ya kimataifa baada ya kuibuka mshindi wa mbio za mita mia nane za IAAF diamond league zilizoaandaliwa mjini Oregon nchini marekani.

Niyonsaba mbali na kuibuka mshindi aliweka rekodi mpya ya mashindano hayo ya dakika moja sekunde hamsini na sita nukta saba mbili, ambayo pia ndio muda wa kasi zaidi duniani mwaka huu katika mbio hizo za mita mia nane kwa kina dada.
Katika mbio za mita elfu tatu kuruka maji za viunzi, Conseslus Kipruto wa KENYA aliwashinda magwiji wa mbio hizo na kuweka rekodi mpya ya mashindano hayo ya dakika nane sekunde tatu nukta tano tisa.
Bingwa wa olimpiki ezekiel kembo alimaliza katika nafasi ya pili naye paul kipsiele akimaliza katika nafasi ya tatu.
Mo Farah
Katika mbio za mita elfu moja mia tano, Silas Kiplagat wa Kenya alimshinda bingwa wa zamani wa Olimpiki Asbel Kiprop kwa kutumia muda wa dakika tatu sekunde 49 nukta tano tatu.
Aman mote wa Ethiopia alimaliza katika nafasi ya tatu.
Mshindi wa medali mbili ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki Mo Farah wa Uingereza, alishindwa katika shindano lake la kwanza mwaka huu katika msururu wa mbio hizo za IAAF Diamond league mita elfu tano.
Farah alimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mshindi wa mbnio hizo mkenya Edwin Soi ambaye alitumia muda wa dakika kumi na tatu na sekunde nne nukta saba tano.
Farah aliamua kushiriki katika mbio hizo za mita elfu tano badala ya mita elfu kumi baada ya kupata matatizo ya kiafya.
Bingwa wa zamani wa Olimpiki Justin Gatlin alishinda mbio za mita mia moja kwa kutumia muda wa sekunda tisa nukta nane nane naye Shelly Ann Fraser wa Jamaica akiibuka mshindi katika mbio hizo za mita mia moja kwa kina dada.
Kenenisa Bekele Mwanariadha wa Ethiopia
Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita elfu kumi, Tirunesh Dibaba alishinda mbio za mita elfu tano naye Kenenisa Bekela akishinda mbio za mita elfu kumi kwa kutumia dakika ishirini na saba na sekunde kumi na mbili.
Awamu ijayo ya mashindano hayo ya diamond league yatafanyika mjini Rome, Italia.

0 comments:

Post a Comment