Wednesday, June 12, 2013

WANA WA PELE WAKUBALI KURUDI TIMU YA TAIFA!!

ANDRE_AYEWRAIS WA NCHI AINGILIA KATI, WAO WAKUBALI KUFUTA MGOMO!!
WANA wa Nguli wa Soka wa Ghana, Abedi Pele, Andre na Jordan Ayew, wamefuta msimamo wao wa kutoichezea Nchi yao baada ya Rais wa Ghana kukutana nao na wao kukubali rai yake kurudia kuichezea Ghana.
Inasemeka Rais wa Ghana, John Dramani Mahama, aliongea na Ghana FA Siku chache zilizopita na kuiuliza ikiwa wanataka msaada wake ili aongee na Mastaa hao
Watoto wa Pele pamoja na Kevin-Prince Boateng na Michael Essien ili wafute uamuzi wao wa kustaafu kuichezea Ghana na FA ilikubali ombi hilo.
KOMBE LA DUNIA-KANDA YA AFRIKA
KUNDI D
[Kila Timu imecheza Mechi 4 bado 2]
Zambia Pointi 10
Ghana 9
Lesotho 2
Sudan 1
**FAHAMU: Timu 1 tu inafuzu hatua ya mwisho ya Mtoano kupata Timu 5 za Afrika zitakazoenda Brazil 2014
MECHI ZIFUATAZO:
-Jumamosi Juni 15: Zambia v Sudan
-Jumapili Juni 16: Lesotho v Ghana
Mapema hii leo, Rais Mahama alikutana na hao Ndu wawili, Andre na Jordan Ayew, ambao wote walikubali ombi la Rais wao la kurudi tena kuitumikia Nchi yao.
Andre Ayew alimuahidi Rais Mahama: “Tumerudi kuitumikia Ghana na kufanya kila juhudi icheze Fainali za Kombe la Dunia.”
Inatarajiwa Kevin-Prince Boateng na Michael Essien pia watakutana na Rais wa Nchi hiyo na pia watabadili msimamo wao.

0 comments:

Post a Comment