Monday, June 10, 2013

Sudan Kusini kuishtaki Sudan kwa UN

Hifadhi za mafuta Sudan Kusini
Sudan Kusini inasema kuwa itawasilisha malalamiko rasmi kwa umoja wa mataifa kuhusu majeshi ya Sudan kuingia katika mipaka yake.

Waziri wa mawasiliano wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin, alisema kuwa majeshi ya Sudan yameingia katika jimbo la Upper Nile ambako majeshi ya Sudan Kusini yaliondoka kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha vita.
Aliongeza kuwa Sudan Kusini italalamikia kikosi cha wanjeshi wa Ethiopia, kinacho shika doria mpakani chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa.
Rais wa SudanOmar al-Bashir, ameamuru kufungwa kwa mabomba yanayosafirisha mafuta kutoka Sudan Kusini kupitia Sudan.Hata hivyo, haijabainika ikiwa Sudan imesitisha usafirishaji huo wa mafuta rasmi.
Waziri Benjamin amesema hatua ya Sudan kufunga mabomba huenda ikaipotozea nchi hiyo mamilioni ya dola inayotokana na uuzaji wa mafuta ghafi.
Naye kwa upande wake, waziri wa mafuta na madini, Stephen Dhieu Dau, alisema kuwa serikali ya Sudan haina uwezo wa kufunga mabomba ya mafuta ya Sudan Kusini itakavyo na hata bila kuonya Juba.
Waziri Dhieu Dau alisema kuwa usafirishaji wa mafuta unafuata maafikiano yaliyotiwa saini na nchi hizo mbili.
Sudan ilichukua hatua ya kufunga mabomba baada ya kudai kuwa Sudan Kusini inaendelea kuunga mkono makundi ya wapiganaji dhidi yake.
Kama ushahidi wake wa kuchukua hatua hiyo, Sudan inasema kuwa Juba inaunga mkono makundi ya wapiganaji wenye kupigia debe mageuzi, mfano, kundi la Terrorist Revolutionary kupitia kwa usaidizi wa jeshi la SPLA.
Sudan inadai kuwa badala ya Sudan Kusini kusitisha msaada wake kwa makundi ya waasi, imeanza kutumia mbinu tofauti kuyasaidia makundi hayo.

0 comments:

Post a Comment