Sunday, June 9, 2013
Real Madrid vs Manchester United,nani mshindi katika hali ya kutafuta saini Cristiano Ronaldo
Vita kali ya usajili inaendelea hivi sasa kati ya klabu za Manchester United na Real Madrid ambapo timu zote mbili zinamuwania mchezaji Cristiano Ronaldo .
Manchester United wana imani kuwa wanaweza kumnunua mchezaji wao wa zamani kwa kiasi cha paundi milioni 65 na upande wa pili wa cita hii Real Madrid wanapambana kuhakikisha Ronaldo anasaini mkataba mwingine utakaomfanya akae zaidi na klabu hiyo.
Ronaldo kwa kauli yake mwenyewe amesema kuwa ana imani kuwa ataendelea kukaa na Real wakati anafanya mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini Hispania lakini bado mabosi wa United wanaamini kuwa watamtambulisha Ronaldo kama mchezaji wa timu yao agosti nane huku akianza kuitumikia United kwenye mechi ya Kumuenzi Rio Ferdinand dhidi ya Sevilla siku moja baadaye .
Wawakilishi wa Ronaldo wanapambana kuhakikisha nyota huyu anasaini mkataba utakaomuingizia paundi milioni 35 kwa mwaka pamoja na asilia 100% ya haki za taswira yake huku mabosi wa Real wakisimamia kwenye ofa yao ya paundi milioni 30 na asilimia 40% mpaka 60% ya haki za taswira yake ambayo itamuingizia ziada ya zaidi ya paundi milioni 20 kwa mwaka . United nao wamemuandalia Ronaldo mshahara wa paundi laki tatu kwa wiki utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa kuliko wote nchini England .
Wadhamini wa Manchester United Nike pamoja na wadhamini wapya Chevrollet wameripotiwa kuwa tayari kusaidia kukusanya fedha zitakazotumika kumnunua Ronaldo ambaye atakuwa mtu muhimu kusukuma kampeni za bidhaa za makampuni hayo .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment