Tuesday, June 11, 2013

NGAO YA JAMII: MAN UNITED v WIGAN KUPIGWA WEMBLEY!

MWAKA JANA ILICHEZWA VILLA PARK!!

MGAO TIKETI: MAN UNITED 35,000 WIGAN 15,000!
NGAO_YA_HISANI_LOGOMWAKA HUU, ule mtanange wa ‘Fungua Dimba’ Msimu mpya wa 2013/14 kati ya Mabingwa wa England, Manchester United, na Washindi wa FA CUP, Wigan Athletics, utachezwa Uwanja wa Wembley Jijini London hapo Agosti 11 kuanzia Saa 10 Jioni.
Mwaka Jana, kwa ajili ya mgongano wa Michezo ya Olimpiki iliyokuwa ikifanyika Jijini London, Mechi hiyo ilibidi ihamishiwe huko Mji wa Birmingham kwenye Uwanja wa Villa Park, Nyumbani kwa Aston Villa.MAN_UNITED-2013-OT
Timu zote mbili zitatinga kwenye Mechi hiyo spesho ya kwanza kabisa kwa Msimu mpya zikiwa na Mameneja wapya kwa Man United kuongozwa na David Moyes aliemrithi Mstaafu Sir Alex Ferguson lakini Wigan hadi sasa haina Meneja mpya baada ya kuondokewa na Roberto Martinez ambae ameenda huko Everton kuchukua wadhifa wa David Moyes.
Akithibitisha Mechi hii, Katibu Mkuu wa FA, Alex Horne, alisema: “Inabidi urudi nyuma hadi Mwaka 1985 ili kuiona Man United wakicheza kwenye Ngao hii bila ya Sir Alex Ferguson! Macho ya kila Mtu yatakuwa kwa David Moyes akiiongoza Man United kwa mara ya kwanza!”
Vile vile, Horne alisema kuwa Mechi hii itakuwa ya mvuto licha ya Wigan Msimu huo mpya kucheza Daraja la chini, Championship, baada kushuka Daraja toka BPL, Barclays Premier League, kwa vile tu iliitwanga Man City kwenye Fainali ya FA CUP.
Hata hivyo, kwa kutwaa FA CUP, Wigan imepata nafasi kucheza Ulaya Msimu wa 2013/14 kwenye Mashindano ya UEFA EUROPA LIGI.
Kila Klabu tayari imetengewa Mgao wake wa Tiketi na Man United watapewa Tiketi 35,000 kuziuza huku Wigan wakipewa Tiketi 15,000 tu na Bei ya Tiket hizo ni kuanzia Pauni 20 hadi 45 [Shilingi 50,900 hadi 114,500].
Akiongelea Mgao huo wa Tiketi, Horne alifafanua: “Washabiki wa Manchester United wanasafiri kwa wingi mno na mgao wa Wigan umefuatia mahudhurio ya Washabiki wao katika Mechi mbili walizocheza Uwanja wa Wembley kwenye FA CUP Msimu uliopita.”
WASHINDI WALIOPITA:
MWAKA
TIMU
2012
Manchester City
2011
Manchester United
2010
Manchester United
2009
Chelsea FC
2008
Manchester United
2007
Manchester United
2006
Liverpool FC
2005
Chelsea FC
2004
Arsenal FC
2003
Manchester United
2002
Arsenal FC
2001
Liverpool FC
2000
Chelsea FC
1999
Arsenal FC
1998
Arsenal FC
1997
Manchester United
1996
Manchester United
1995
Everton FC
1994
Manchester United
1993
Manchester United
1992
Leeds United
1991
Tottenham Hotspur
1991
Arsenal FC
1990
Liverpool FC
1990
Manchester United
1989
Liverpool FC
1988
Liverpool FC
1987
Everton FC
1986
Liverpool FC
1986
Everton FC
1985
Everton FC
1984
Everton FC
1983
Manchester United
1982
Liverpool FC
1981
Tottenham Hotspur
1981
Aston Villa
1980
Liverpool FC
1979
Liverpool FC
1978
Nottingham Forest
1977
Liverpool FC
1977
Manchester United
1976
Liverpool FC
1975
Derby County
1974
Liverpool FC
1973
Burnley FC
1972
Manchester City
1971
Leicester City
1970
Everton FC
1969
Leeds United
1968
Manchester City
1967
Manchester United
1967
Tottenham Hotspur
1966
Liverpool FC
1965
Liverpool FC
1965
Manchester United
1964
West Ham United
1964
Liverpool FC
1963
Everton FC
1962
Tottenham Hotspur
1961
Tottenham Hotspur
1960
Wolverhampton Wanderers
1960
Burnley FC
1959
Wolverhampton Wanderers
1958
Bolton Wanderers
1957
Manchester United
1956
Manchester United
1955
Chelsea FC
1954
Wolverhampton Wanderers
1954
West Bromwich Albion
1953
Arsenal FC
1952
Manchester United
1951
Tottenham Hotspur
1950
England
1949
Wolverhampton Wanderers
1949
Portsmouth FC
1948
Arsenal FC
1938
Arsenal FC
1937
Manchester City
1936
Sunderland AFC
1935
Sheffield Wednesday
1934
Arsenal FC
1933
Arsenal FC
1932
Everton FC
1931
Arsenal FC
1930
Arsenal FC
1929
English Professionals
1928
Everton FC
1927
Cardiff City
1926
English Amateurs
1925
English Amateurs
1924
English Professionals
1923
English Professionals
1922
Huddersfield Town
1921
Tottenham Hotspur
1920
West Bromwich Albion
1913
English Professionals
1912
Blackburn Rovers
1911
Manchester United
1910
Brighton & Hove Albion
1909
Newcastle United
1908
Manchester United

0 comments:

Post a Comment