Thursday, June 13, 2013

KOMBE LA DUNIA: NIGERIA YANUSURIKA WINDHOEK!

KUNDI F ATAKAESONGA NI NIGERIA AU MALAWI.
SEP 6 KUAMUA, NI MTANANGE NIGERIA V MALAWI
JANA huko Windhoek, Nigeria walinusurika kichapo toka kwa Namibia katika Mechi ya KUNDI F la Kombe la Dunia 2014 Kanda ya Afrika walipotoka Sare ya 1-1 lakini bado wako kileleni Pointi 2 mbele ya Malawi ambao mapema jana walitoka 2-2 na Kenya huko Lilongwe.
Matokeo hayo yanafanya Timu moja ambayo itasonga Raundi ya Mtoano ya Timu 10
ambayo itatoa Washindi watano watakaoenda Brazil Mwaka 2014 kuamuliwa hapo Septemba 6 zitakapochezwa Mechi za mwisho za Kundi kwa Nigeria kucheza na Malawi na Kenya kucheza na Namibia.
KUNDI F
Nigeria –Pointi 9
Malawi - Pointi 7
Namibia -Pointi 5
Kenya - Pointi 3
MECHI ZA MWISHO:
Septemba 6
Nigeria v Malawi
Kenya v Namibia
Super Eagles walinusurika kipigo baada ya Godfrey Oboabona kusawazisha Bao zikiwa zimebaki Dakika 7 baada ya Deon Hotto Kavendji  kuifungia Namibia Bao katika Dakika ya 77 kwenye Mechi kali iliyochezwa Sam Nujoma Stadium huko Mjini Windhoek.
Nigeria sasa wanasafiri kwenda huko Brazil kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayoanza Juni 15 na wao kufungua dimba na Tahiti hapo Juni 17 kwenye Mechi ya KUNDI B.
MAGOLI:
Malawi 2
-46' Ngalande
81' Ng’ambi
Kenya 2
52' Mohammed
89' Kayira [Kajifunga mwenyewe]
Namibia 1
77' Hotto
Nigeria 1
83' Godfrey Oboabona
Mapema huko Lilongwe, Malawi waliikosa Kenya baada ya Mchezaji wao Kayira kujifunga mwenyewe na kuipa Kenya Sare ya Bao 2-2.
Kenya na Namibia hazina nafasi tena ya kufuzu kutoka KUNDI F.

0 comments:

Post a Comment