Bara la Asia litaingiza moja kwa moja
Timu 4 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, mbili toka kila Kundi la
michuano yao, na Timu ya 5 itapatikana baada ya Timu zitazoshika Nafasi
za 3 kwenye Makundi kucheza Mechi kati yao na Mshindi kwenda kucheza na
Timu kutoka Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini itakayomaliza Nafasi ya
5.
Kesho Jumanne Juni 4, Japan, wanaoongoza
Kundi B wakiwa na Pointi 13, watakuwa Nyumbani kucheza na Australia na
wanahistaji sare tu ili watinge Brazil na kuwa Nchi ya kwanza Duniani
kufanya hivyo lakini pia hiyo kesho wanaweza kuingia Fainali hata
wakifungwa ikiwa tu Iraq, wanaocheza Ugenini, watashindwa kuifunga Oman.
Japan wangeweza kufuzu kwenda Brazil
kwenye Mechi za Raundi iliyopita lakini walifungwa 2-1 bila kutegemewa
walipocheza Ugenini na Jordan lakini Mechi hii na Australia,
itakayochezwa huko Saitama World Cup Stadium ni ngumu kwa vile Australia
wana Wachezaji wazoefu na wao wanasaka ushindi ili nao waweze kufuzu.
Matumaini ya Japan yapo kwa Wachezaji
wao kina Keisuke Honda, Yuto Nagatomo na Shinji Kagawa huku Australia
ikitegemea Kikosi chao chenye Wachezaji wakongwe ambao nusu yao wako
kwenye Umri unaozidi Miaka 30.
Katika Mechi yao ya kwanza kwenye Kundi lao Timu hizi zilitoka sare ya Bao 1-1.
RATIBA MECHI ZILIZOBAKI:
Jumanne Juni 4
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
13:30 Japan v Australia [1-1]
13:00 Oman v Iraq [1-1]
16:15 Qatar v Iran [0-0]
17:30 Lebanon v South Korea [0-3]
Jumanne Juni 11
8:00 Australia v Jordan [1-2]
11:00 South Korea v Uzbekistan [2-2]
14:30 Iraq v Japan [0-1]
16:30 Iran v Lebanon [0-1]
Jumanne Juni 18
11:00 Australia v Iraq [2-1]
15:00 South Korea v Iran [0-1]
15:00 Uzbekistan v Qatar [1-0]
19:00 Jordan v Oman [1-2]
MSIMAMO:
KUNDI A
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Uzbekistan |
6 |
3 |
2 |
1 |
6 |
4 |
2 |
11 |
2 |
South Korea |
5 |
3 |
1 |
1 |
11 |
5 |
6 |
10 |
3 |
Iran |
5 |
2 |
1 |
2 |
2 |
2 |
0 |
7 |
4 |
Qatar |
6 |
2 |
1 |
3 |
4 |
7 |
-3 |
7 |
5 |
Lebanon |
6 |
1 |
1 |
4 |
2 |
7 |
-5 |
4 |
KUNDI B
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Japan |
6 |
4 |
1 |
1 |
14 |
4 |
10 |
13 |
2 |
Jordan |
6 |
2 |
1 |
3 |
6 |
12 |
-6 |
7 |
3 |
Australia |
5 |
1 |
3 |
1 |
6 |
6 |
0 |
6 |
4 |
Oman |
6 |
1 |
3 |
2 |
6 |
9 |
-3 |
6 |
5 |
Iraq |
5 |
1 |
2 |
2 |
4 |
5 |
-1 |
5 |
0 comments:
Post a Comment